Robert anasema kuna usemi mmoja unasema kwamba wafanyakazi wanafanya kazi kwa bidii sana ili wasifukuzwe, waajiri wanalipa kidogo sana kiasi kwamba wafanyakazi hawataacha kazi. Ukiangalia malipo ya makampuni mengi usemi huo una ukweli sana na ndio maana wafanyakazi wengi hawawezi kupata maendeleo makubwa. Na wao bila ya kujali tatizo ni nini wanafanya kile ambacho wameambiwa kwa muda mrefu, pata kazi nzuri na yenye usalama. Anasema wafanyakazi ambao wanaangalia kile wanachopata kwa muda mfupi huwa na wakati mgumu sana baadae.
Robert anashauri vijana ambao wanatafuta kazi watafute kazi ambayo watajifunza na sio kuangalia tu kipato. Waangalie ajira ambayo wanaweza kujifunza na baadae kutumia elimu na uzoefu huo kwenye biashara zao wenyewe. Hata kwa watu ambao tayari wameshaingia kwenye ajira Robert anawashauri kutafuta kazi nyingine ya ziada ambayo itawawezesha kujifunza zaidi. Mara nyingi anawashauri wafanyakazi wajiunge na biashara ya mtandao(network marketing) ambapo wataweza kujifunza jinsi ya kuuza, jinsi ya kutafuta soko la bidhaa na pia kumfanya mtu kuweza kushinda woga na hofu ya kushindwa. Anasema baadhi ya kampuni zinazofanya biashara kwa njia hii wana mafundisho mazuri sana kwa wanaojiunga nazo.
Robert huwa anawauliza wanafunzi wake ni nani anaweza kupiga mkate wa nyama mzuri kuliko kampuni ya McDonalds ambayo inasifika kwa vyakula hivyo? Wanafunzi karibu wote husema wanaweza kupika vizuri zaidi ya kampuni hiyo. Robert anawauliza kwa nini na nyie sio tajiri kama McDonalds ili hali mnaweza kupika mikate ya nyama mizuri zaidi? Jibu ni kwamba watu wanajua kupika mikate vizuri ila McDonalds wana mfumo mzuri wa kuwez akuuza mikate yao na hivyo kupata faida kubwa.
Hivyo na wewe acha kungangania kile unachokijua tu bali jifunze zaidi kuhusu mfumo wa biashara ambao utakuwezesha uweze kuuza zaidi na kufikia mafanikio. Robert anasema dunia imejaa watu wenye vipaji sana ila ni masikini.Anasema watu hawa wanateseka sio kwa kile wanachokijua bali kwa kile ambacho hawakijui. Hii ni kwa sababu watu hawa wanaweza kufanya kazi zao vizuri sana ila hawajui jinsi ya kuziuza na kutengeneza biashara kubwa.
Robert anasema makampuni makubwa hutengeneza watu watakaokuja kuongoza makampuni hayo baadae. Watu hawa hawafanyi kazi kwenye idara moja tu, bali huhamishwa kwenye kila idara ili kujifunza kila eneo linalohusiana na kampuni hiyo. Anasema hata matajiri wanafanya hivi, kuwafanya watoto wao wajue mambo mengi kuhusu biashara.
Robert anasema kuchagua kazi kwa kigezo cha kujifunza badala ya fedha inaweza isikulipe sana mwanzoni ila baadae itakuwa faida kubwa sana kwako.
Maeneo matatu yanayohitaji usimamizi mzuri kwenye biashara.
Maeneo muhimu unayotakiwa kujua jinsi ya kusimamia ili uweze kufikia mafanikio kwenye biashara ni;
1. Usimamizi wa mzunguko wa fedha.
2. Usimamizi wa mfumo wa biashara ikiwemo wewe mwenyewe na muda wako wa kazi na wa familia.
2. Na usimamizi wa watu.
Ujuzi mwingine mkubwa unaotakiwa kuwa nao ni mauzo(sales) na masoko(marketing). Ni uwezo wa kuuza ndio utakaokuwezesha kufikia mafanikio.
Robert anasema siku hizi anakutana na walimu wa zamani ambao sasa hivi wana maisha mazuri kuliko walipokuwa wanafundisha tu baada ya kujifunza mambo ya ziada kuhusu biashara.
Jinsi ya kuanza.
Robert anasema angetamani kusema kupata utajiri ilikuwa rahisi kwake ila sio kweli. Anasema kwenye kujibu swali linaloulizwa na watu wengi kwamba NITAANZAJE? Anawashauri kutumia mfumo ambao anautumia yeye kila siku. Robert anasema kuna mawazo mengi sana ya biashara, na ni rahisi kuyapata. Ila kupata wazo zuri ambalo litakuletea mafanikio makubwa unatakiwa kubadili kwanza mfumo wako wa kufikiri ambao unakuandaa kuwa mwajiriwa na baadae kustaafu. Robert anashauri hatua kumi muhimu unazoweza kuzitumia kama sehemu ya wewe kuanza. Tutajifunza hatua hizi kwenye makala ijayo.
Tunajifunza nini hapa?
1. Katika ajira, mafanyakazi anaumia kwa kufanya kazi sana, wakati mwajiri anafaidiak kwa kulipa mshahara kidogo sana.
2. Ni vyema kutafuta kazi ambayo utajifunza badala ya kutafuta kazi ambayo utapata tu fedha.
3. Ni muhimu kujifunza kupitia kazi ili kuweza kutumia elimu hiyo kwenye biashara.
4. Kama umeajiriwa na unataka kujifunza biashara ukiwa bado kwenye ajira yako jiunge na kampuni inayofanya biashara kwa njia ya mtandao(Network marketing).
5. Ili ufanikiwe kupitia biashara ni lazima uweze kuwa na usimamizi mzuri kwenye mzunguko wa fedha, mfumo wa biashara na watu.
6. Ni muhimu sana kujua kuuza(sales) na kutafuta masoko(marketing) ili uweze kufanikiwa kwenye biashara.
Nakutakia kila la kheri kwenye mafanikio ya biashara yako.
TUKO PAMOJA.
ahsante naomba maelekezo ya kujiunga na network marketing
LikeLike
Sawa, nitakutumia email ya maelekezo.
Karibu sana.
LikeLike
Asante Amani.
Na mimi naomba maelekezo ya Network marketing
LikeLike
Tayari nimekutumia, Karibu sana.
LikeLike
na mimi naomba maelekezo ya kujiunga na network marketing
LikeLike
Tayari nimekutumia, Karibu sana.
LikeLike