Mtu aliyetamani kuingia kwenye ubia na Thomas A. Edison.
Ni kweli kwamba mawazo ni vitu ambavyo kama vikichanganywa na malengo, uvumilivu na shauku kubwa lazima yatamfikisha mtu kwenye utajiri wa mali. Edwin C Barnes alitamani sana kuingia kwenye ybia naThomas Edison(Thomas Edison alikuwa mwanasayansi na mgunduzi mkubwa sana wa enzi hizo. Na pia alikuwa tajiri mkubwa kutokana na uvumbuzi wake. Huyu ndiye mtu aliyegubdua taa ya umeme licha ya kushindwa mara elfu moja). Lengo la Edwin halikuwa kuwa mfanyakazi wa Edison, bali kufanya nae kazi kama mshirika wake. Hakuwa anamjua Edison na hakuwa hata na nauli ya kuweza kusafiri mpaka kufika vilipo viwanda vya Edison, lakini hilo halikumkatisha tamaa. Hitaji lake hili lilimsukuma sana na aliamua kusafiri kwa treni ya mizigo mpaka kufika kwenye maabara ya Edison. Alipofika pale alimwambia Edison kwamba anataka kufanya nae kazi na awe mshirika wake. Edison alimwangalia kwa mshangao kwa sababu alionekana ni kijana aliyechoka na maisha. Lakini aliona kitu fulani kwenye sura yake kilichomshawishi kwamba alikuwa kweli anamaanisha alichosema.
Edwin alipewa kazi kama msaidizi wa Edison na alikuwa anamsaidia Edison kazi ambazo hazikuwa muhimu kwake. Alikuwa analipwa mshahara kidogo sana lakini hilo halikumfanya asahau lengo lake kubwa. Miezi ilienda bila ya mabadiliko yoyote, lakinialiendelea kujifunza na kuwa mvumilivu.
Siku moja fursa ilikuja upande wa Edwin, Edison alikuwa maetengeneza mashine moja iliyokuwa inajulikana kama ediphone, baada ya kuwapa wauzaji wauze mashine ile hawakuipenda na walimwambia haiwezi kuwa na soko.Edwin alimwambia Edison kwamba anaweza kuuza mashine hiyo na akapewa nafasi hiyo. Aliweza kuuza mashine hiyo kwa mafanikio sana kiasi kwamba Edison alimpatia mkataba wa kuuza mashine hiyo kwa nchi nzima. Na hapo ndipo ushirika wao ulipoanzia. Ushirikiano ambao ulidumu kwa miaka zaidi ya 30 na wote walinufaika sana.
Edwin hakuwa na chochote cha kuanzia bali shauku kubwa ya kufanikiwa. Alijua ni kitu gani anataka na hakukubali kupoteza muelekeo wake. Na hatimaye alikipata.
Futi tatu kutoka kuifikia dhahabu.
Moja ya sababu za kushindwa ni tabia ya kukata tamaa pale mtu anapokutana na changamoto au vikwazo. Kila mtu amewahi kufanya hivi katika wakati fulani kwenye maisha yake, na hujutia kitu hiko. Mjomba wa bwana mmoja aliyekuwa anajulikana kama R. U. Darby, alipata taarifa ya kupatikana kwa madini ya dhahabu kwenye eneo alilopo. Alikwenda kuchimba madini yale na baada ya kuchimba kidogo alikutana na mwamba mkubwa sana wa madini. Alipata shauku kubwa na akaenda kuwaeleza ndugu zake na haraka sana wakachanga fedha na kwenda kununua vifaa vya uchimbaji. Darby na mjomba wake walienda kwenye eneo la mgodi na baada ya kuchimba kidogo mwamba ule wa madini uliisha. Waliendelea kuchimba na kuchimba lakini hawakukuta madini. Wakaendelea kuchimba tena na tena bila ya matumaini yoyote. Baadae wakakubali kwamba eneo lile halina madini tena na hivyo kuuza vifaa vyote na kuondoka zao.
Yule aliyenunua vifaa vile alienda kumuita mtaalamu wa miamba na kumwambia achunguze kama kutakuwa na mwamba wa madini pale. Baada ya uchunguzi waligundua mwamba wa madini ulikuwa futi tatu tu kutoka pale walipoishia wale mabwana. Mtu yule alipata utajiri mkubwa sana kwa madini yale. Baada ya Darby kusikia habari ile alifanya maamuzi kwamba hatokuja kukata tamaa kwenye jambo lolote na maamuzi haya yalimfanya aweze kufanikiwa sana kwenye biashara ya kuuza bima.
Kwa hadithi hizi mbili kuna mambo mengi sana ya kujifunza. Na kupitia kitabu hiki tutajifunza sheria kumi na sita muhimu za kuweza kutufikisha kwenye mafanikio makubwa ya fedha na mali.
Nini cha kujifunza?
Katika sehemu hii ya uchambuzi umejifunza nini. Hadithi hizo mbili ni za kweli na zilitokea kipindi cha nyuma ambapo kitabu huki kimeandikwa. Ila mpaka leo tunaona watu wakifanya makosa yale yale na kuwazuia kufikia mafanikio. Tushirikishe mambo matano uliyojifunza kwenye sehemu ya leo ya uchambuzi hapo chini. Kumbuka unapoandika yale uliyojifunza ni rahisi zaidi kuyafuata kuliko mimi nikikuandikia hapo.
Hivyo tushirikishane mambo matano tuliyojifunza.
Karibuni.
mambo zaid ya matano yalopo kwenye uchambuz huu.1@ tujitume kwenye kazi za kimafanikio.2@.hakuna linaloshindikana katka mafanikio.3@.tuwe na uvumilivu.4@tuwe na shauku.5tutafite wataalamu au washaur katka kazi za kimafanikio.6kusaka mafanikio hakuna mwsho na wala hakujaaaza leo hivyo tuendeleze jukum hilo.7@tujiepushe na kukata tamaa..tufanye kazi kwa malengo
LikeLike
Asante sana Godlove.
LikeLike
Unapotaka kufanya jambo ambalo huna utaalam nalo shirikisha wataam ndipo juhudi zingine zifuate.
Unapoamua kufanya jambo fanya kwa moyo wote na uckatishwe tamaa na ugumu wa jambo.
Unapotaka kujifunza jambo kwa aliyefanikiwa kua tayari kujifunza na si kuangalia masilahi ya muda mfupi.
Katika mafanikio kitu muhim ni kujua unakotaka kwenda (wazo na shauku)na si kutishwa na hali uliyo nayo ama namna ya kufika.
Tusiwagope watu waliofanikiwa kwani wengi wao hua tayari kumsaidia mwenye shauku ya dhati ya kutaka kujifunza juu ya mafanikio.
LikeLike
Asante Ibrahim.
LikeLike
ukiamua kujifunza ondoa woga au hofu ya kuomba ushauri kwa wajasiliamali mali wakubwa eti kwa kuwa atakuona sio wa level zake, mfano mzuri mimi nilienda kwa mmiliki wa makampuni ya IPP kuomba ushauri fulani japo nilinyanyaswa sana na watumishi lakini sikukata tamaa ndipo nilipoenda nyumbani kwake baada ya juhudi za kuonana ofisini kwake kugonga mwamba, NEVER GIVE UP. you never know .
LikeLike
Asante sama Zanuni.
Ulifanikiwa kuonana naye?
LikeLike
Mambo matano niliyojifunza
1.Unachokiwaza na kukiamini ndani yako huwa kinaonekana hata kwa taswira ya nje,kama Edson alivomtazama Edwin aligundua shauku anayoiwaza na kuiamini kuwa anaweza kuitimiza akipewa nafasi
2.Kutokata tamaa katika kuelekea safari ya mafanikio
3.Tusiongope vikwako katika maisha ni sehemu ya mitihani ya kuelekea kwenye mafanikio tuendelee kujifunza
4.Daima usiyumbe wala kuteteleka katika dira ya kuelekea kwenye mafanikio wewe fanya tu haijalisi uko katika hali gani
5.Kila wakati ongeza juhudi ya kufanya kazi kwa kujiboresha kifra,mbinu mpya zinazoweza kukupa ushindi.
LikeLike
Asante sana kwa kutushirikisha uliyojifunza.
Yafanyie kazi.
LikeLike
Katika uchambuzi huu nimeona kuna umuhimu mkubwa sana wa kujifunza namna ya kuuza i.e sales skill,kwani wauzaji walimwambia Thomas Bidhaa yake haiwezi kuuzika lakini Edwin aliuza bidhaa hiyo hiyo kwa mafanikio
LikeLike
Vizuri sana,
Fanyia kazi hilo ili uweze kuuza zaidi.
LikeLike