Akili ya binadamu imegawanyika katika sehemu tatu, kuna akili inayofikiri na kufanya maamuzi (conscious mind), kuna akili isiyofikiri wala kufanya maamuzi ila inapokea kila taarifa inayoingizwa(subconscious mind) na kuna akili ya juu kabisa inayotawala akili hizi(superconscious mind).
Akili ya ndani ambayo haifanyi maamuzi ina nguvu kubwa sana ya kuwez akupokea kila taarifa inayoingia kwenye akili yako. Na akili hii hutumua taarifa zinazojirudia rudia katika na kutengeneza mazingira ya kuwezesha mambo hayo kutokea. Hii ndio maana mtu anayewaza kushindwa kwenye kila kitu huishia kushindwa na yule anayewaza kushinda kila siku hushinda kwenye kila jambo analofanya.
Sasa hatua ya nne ya kufikia utajiri kama ambavyo imefundishwa kwenye kitabu hiki THINK AND GROW RICH ni kuweza kuiamrisha akili yako ya ndani ili ikutengenezee mazingira yatakayokuwezesha kufikia utajiri.
Njia inayotumika kwenye kuamrisha akili yako ya ndani ni kujitengenezea mawazo ambayo utakuwa unayawaza kila siku na kujitengenezea kauli ambayo utakuwa unajiambia kila siku. Njia hii kwenye kitabu imeitwa kama AUTO-SUGGESTION, yaani kujijengea mawazo wewe mwenyewe ambayo yatakuwezesha kufikia utajiri.
Binadamu anao uwezo mkubwa wa kuamua ni mawazo gani yaingie kwenye akili yake ya ndani. Kwa kuweza kutumia uwezo huu na kuweka mawazo ambayo yanakujengea uwezo na kukuweka kwenye mazingira ya kupata utajiri itakuwezesha kufikia utajiri.
Kumbuka tuliona kwamba akili yako ya ndani ni kama shamba lenye rutuba. Shamba hili lisipolimwa magugu huota na kutawala. Ila shamba hili linapolimwa vizuri hutoa mazao mazuri sana. Hivyo hivyo unapoacha subconscious mind yako iingiliwe na mawazo yasiyo na maana mambo hayo yasiyo na maana ndio yanatokea kwenye maisha yako. Ila ukiweza kudhibiti akili yako hii na kuingiza mawazo ambayo ni ya kukujenga utaweza kufikia hicho unachotaka.
Kumbuka pia tulipitia hatua sita za kuandika kauli ambayo utakuwa unaisoma kila siku asubuhi unapoamka na kila siku usiku kabla ya kulala. Yote haya ni katika kuhakikisha akili yako kwa wakati wowote inakuwa na mawazo ya kukufikisha wewe kwenye utajiri na hivyo kukuwezesha wewe kuziona na kuzitumia fursa zinazokuzunguka na kukuletea utajiri. Endelea na zoezi lile kila siku ili kuweza kuiweka akili yako katika hali ya kukuwezesha kufikia utajiri. Kumbuka wakati unafanya hivi useme kwa hisia maana hisia zitawezesha akili yako ya ndani kuchukua mawazo hayo kwa msisitizo mkubwa.
Unahitaji kuweka mawazo ya kile unachotaka kwenye akili yako na kwa hisia kazi kiasi kwmaba hili linakuwa ndio hitaji lako kubwa kwenye maisha. Kwa kulifanya kuwa hitaji kubwa inakufanya uweze kulipigania na kutokukata tamaa kwa sababu utakuw ana uhakika wa kulifikia. Wakati unasema kauli yako ya kufikia utajiri, zione fedha zikiwa zinakuzunguka, weka hisia kwamba unazo tayari na kuwa na imani kwamba tayari unacho kile unachotaka.
Baada ya kuwa na mawazo haya kwenye akili yako, pia unahitaji kuchukua hatua na kufanya kazi ili unayotaka yaweze kutokea. Kumbuka hutapata fedha kwa kesema na kufikiria fedha kila siku, pamoja na hatua hiyo muhimu unahitaji kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ndio uweze kupata fedha hizo. Kwa kuwa na mtazamo huu sahihi kutakuwezesha wewe kuona fursa nyingi zaidi za kifedha kupitia kile unachofanya. Wakati unasema kwa hisia na kuziona fedha zikikuzunguka, pia tengeneza picha ya wewe ukitoa huduma au bidhaa ambazo zinawasaidia wengine na wao wanakulipa kwa hilo. Hii ni muhimu sana ili uweze kufanya kazi bora na kupata kipato kikubwa kitakachokufikisha kwenye utajiri.
Kwa mawazo ya kawaida unaweza kuona kufanya hivi sio muhimu au ni kupoteza muda ila ni muhimu sana katika kuijenga akili yako kuweza kukufikiasha kwenye mafanikio. Pia kunakuwezesha kuondokana na mtizamo na mawazo hasi ambayo yangekuwa kikwazo kwako kuweza kufikia utajiri ambao unautarajia kwenye maisha yako. Kumbuka hutaki utajiri huu kw akuwaibia wengine, ila unautaka kwa kutoa huduma au bidhaa bora ambazo zinawasaidia wengine pia.
Kumbuka kupitia hatua zile sita na kutamka kauli yako kila siku kabla ya kulala, ili unapolala subconscious mind yako ifanyie kazi mawazo yako. Na pia iseme kauli hiyo kabla ya kuianza siku ili subconscious mind yako iweze kukuonesha fursa mbalimbali kila siku za kukuwezesha kufikia utajiri.
Nakutakia kila la kheri kwenye maisha yako ya kitajiri ambayo umeshayafikia.
TUPO PAMOJA.