Kama unataka kufikia mafanikio makubwa sana kw akiwango cha world class kwanza kabisa unahitaji kuwa kiongozi mzuri. Kiongozi sio lazima uwe kwenye siasa, bali biashara unayofanya unahitaji kuwa kiongozi ili uweze kufanikiwa sana. Unahitaji kuweza kuwaongoza mbali mbali ili kuweza kuifikisha biashara yako ngazi za juu sana.
Leo hapa tutajifunza sifa 11 muhimu unazotakiwa kuw anazo ili kufanikiwa sana kwenye uongozi na hatimaye kufikia mafanikio makubwa kwenye kile unachofanya.
1. Ujasiri usioyumbishwa. Ili uweze kuwa kiongozi mzuri unahitaji kuwa na ujasiri mkubwa na usioyumbishwa. Unatakiw akujiamini mwenyewe na kuw ana uhakika kwmaba kitu unachofanyia kazi hutokata tamaa. Hakuna mtu anayekubali kuongozwa a mtu ambaye sio jasiri. Kuwa jasiri, jiamini na wengine watajisikia usalama wakiwa chini yako.
2. Kuweza kujidhibiti. Mtu ambaye hawezi kujidhibiti mwenyewe, hawezi kuwadhibiti wengine. Unapoweza kujidhibiti, unapoweza kujiongoza unawavuta wengine nao wawe chini ya uongozi wako.
3. Haki na usawa. Kiongozi anayefanikiwa ni yule anayetoa haki na usawa kwa wote bila ya upendeleo. Kushindwa kufanya hivi kutakuangusha wewe kama kiongozi.
4. Maamuzi Yasiyoyumbishwa. Mtu ambaye anabadili badili maamuzi yake kila mara anaonesha kwmaba hajiamini na hawezi kuwaongoza watu wengine. Kama kiongozi unatakiwa kufanya maamuzi ambayo utaweza kuyasimamia.
5. Mipango mizuri. Kiongozi bora huweka mipango ya kazi yake na hufanya kazi kwa mipango yake. Mtu ambaye anafanya kazi tu bila ya mipango yoyote mara nyingi hujikuta kwenye wakati mgumu. Huwezi kufanikiwa kwenye uongozi kama huna mipango ya kazi zako.
6. Kufanya zaidi ya unavyolipwa. Sifa nyingine muhimu ya kufanikiwa kama kiongozi ni kufanya zaidi ya unavyolipwa. Kufanya zaidi ya kile ambacho unategemew kufanya imawafanya watu wegine wakuamini zaidi na hivyo kuwa kiongozi bora.
7. Haiba nzuri. Hakuna mtu asiyejali anayeweza kufanikiwa kwenye uongozi. Kama unataka kuwa kiongozi bora unahitaji kuwa na haiba nzuri na ya kuweza kuwavutia wengine.
8. Huruma na kuelewa. Kiongozi bora ni yule ambaye anawaelewa watu anaowaongoza na pia kuw ana huruma. Kiongozi anahitaji kujua matatizo ya watu wake na kuwaonesha kwmaba yupo pamoja nao katika kutatua matatizo hayo.
9. Kujua kile unacofanya. Kiongozi bora ni yule ambaye anajua kile anachofanya kwa undani sana.
10. Kukubali majukumu. Kiongozi bora ni yule ambaye yupo tayari kukubali majukumu hata pale wengine wanapokosea. Kama kiongozi anakimbia majukumu yake au kuyakataa basi hawezi kufanikiwa. Na kama mtu wa chini yake amefanya makosa kwa kutokujua kiongozi bora huchukulia hayo kama makosa yake yeye.
11. Ushirikiano. Kiongozi bora ni yule ambaye anaweza kujenga ushirikiano mzuri baina yake na wale anaowaongoza na kuweza kuhumiza ushirikiano baina ya watu wake. Kiongozi anahitaji kuw ana nguvu ya ushawushi na nguvu hii inatokana na ushirikiano.
Unahitaji kuwa kiongozi kwenye maisha yako, unahitaji kuwa kiongozi kwenye biashara yako. Jijengee sifa hizi 11 na utafanikiwa sana kwenye uongozi wako.
Nakutakia kila la kheri.
TUPO PAMOJA.