Jana kwenye mbinu ya biashara tuliangalia mwisho wa ufalme wa mteja. Tuliona ni wakati gani ambapo mteja anaacha kuwamfalme na umuhimu wa kujua hilo. Kama hukupata nafasi ya kusoma makala ya jana isome hapa; BIASHARA LEO; Mwisho Wa Ufalme Wa Mteja.

Leo tutaangalia wateja ambao unatakiwa kuwafukuza mara moja. Wateja hawa wamekuwa mzigo kwako na wanachangia biashara yako kutokufanya vizuri.

Je ni wateja gani ambao unatakiw akuwafukuza? Hawa ni wateja ambao tuliwajadili jana ambao wameshaondoka kwenye kundi la wateja ambao ni wafalme.

Hawa ni wateja ambao wanakuletea matatizo mengi kuliko faida unayoipata kupitia wao.

Utawajuaje wateja hawa?

Njia rahisi ya kuwajua wateja hawa ni kutumia sheria ya 80/20. Sheria hii inasema kwamba asilimia 80 ya faida yako kwenye biashara inatokana na asilimia 20 ya wateja wako. Na pia asilimia 80 ya matatizo yanayotokana na wateja yanatoka kwenye asilimia 20 ya wateja wako. Sasa ni jukumu lako kujua silimia hii 20 ya wateja ambao wanaleta matatizo kwa asilimia 80. Kisha unawaangalia wateja hao na kuona ni wapi ambao unaweza kuwapunguza.

Najua hili linaweza kuwa gumu sana kwako kwa kuona kama kufukuza mteja mmoja umepoteza kila kitu. Lakini yanaweza kuwa maamuzi sahih sana kwako kufanya. Unahitaji kufanya biashara na wateja ambao wanakuamini, wanakuheshimu na wewe unawachukulia hivyo hivyo. Kama kuna mteja kwa sababu zake binafsi anakuchukulia wewe ni wa hovyo, mfukuze haraka kabla hajaharibu biashara yako.

SOMA; Tabia Saba Za Watu Wasiokuwa Na Mafanikio.

Naposema ufukuze mteja simaanishi ufanye hivyo kwa hali ya ugomvi, ila tumia busara zako kuona ni jinsi gani mteja huyo ataacha kufanya biashara na wewe. Na utakapotumia njia hizi, mteja anaweza hata kubadilika na kuona makosa aliyokuwa akiyafanya.

Nakutakia mafanikio kwenye biashara yako.

Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.

SOMA; Huyu Ni Mjasiriamali Mwenye Hamasa Kubwa sana. Unaweza kujifunza kila kitu kutoka kwake.