Mbinu bora kabisa itakayokuwezesha wewe kufanya biashara yako wka mafanikio ni kubadili mtazamo wako katika biashara unayofanya.

Tulishakubaliana kwamba lengo la biashara sio kupata faida bali kutengeneza wateja wa kudumu, kama tulivyoona hapa; Lengo La Biashara Sio Kupata Faida, Bali Ni Hili Hapa.

Sasa leo tutajifunza mbinu nyingine muhimu ambayo ni kubadili jinsi unavyoichukulia biashara yako. Usiichukulie biashara yako kama tu ni kuuza na kununua bali chukulia biashara hiyo kama kutatua matatizo ya watu.

Kama unauza chakula basi jua kwamba unatatua tatizo la njaa. Kama unauza magari basi jua unatatua tatizo la usafiri. Kama unauza vitu vya ndani basi unatatua tatizo la malazi na kadhalika.

SOMA; Huu Ndio Mtaji Mkubwa Ambao Tayari Unao.

Ni nini faida ya kufanya biashara kwa mtazamo wa kutatua matatizo? Hii itakuwezesha wewe kuweza kujenga mahusiano mazuri na wateja wako. Kama unatatua tatizo la njaa, utampatia mteja kile ambacho kweli kutamuondolea njaa yake. Kama unatatua tatizo la usafiri basi utampatia mteja wako gari au usafiri utakaoweza kumuondolea tatizo hilo. Kadhalika kwenye tatizo la malazi, utampatia mteja bidhaa au huduma zitakazomfanya afurahie malazi yake.

SOMA; Kila Suluhisho Linatengeneza Tatizo, Chagua Ni Tatizo Gani Unataka.

Kwa mtazamo huu utakuwa unakazana kutoa bidhaa au huduma ambayo ni bora sana kwa mteja wako na mteja ataendelea kufanya biasahara na wewe kwa muda mrefu. Na pia atakuwa tayari kuwaambia wateja wengine kuhusu biashara yako, na hivyo utakuwa umevuka changamoto hii ya Kwa Nini Watu Hawawaambii Wengine Kuhusu Biashara Yako.

Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.

Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.