Nimekuwa napata bahati ya kukutana na kuwasiliana na wafanyabiashara wengi wadogo na wa kati kwa ajili ya ushauri. Kitu kikubwa ambacho nimekuwa nakiona ni mtazamo wa mtu kwenye biashara una athari kubwa sana kwenye biashara ya mtu.

Kuna watu ambao wanafanya biashara kwa sababu wanataka tu kupata faida. Hawa ni watu ambao hawajali sana kuhusu ukuaji wa biashara wanayofanya, wanachoangalia ni faida. Na watu hawa wanakuwa na wakati mgumu sana kwenye biashara zao.

SOMA; Usipige Kelele, Fanya Watu Waone…

Kuna wengine ambao wanachukulia biashara kama sehemu ya kujishikiza. Labda amesoma ila hajapata kazi bado, hivyo wakati anaendelea kuomba kazi anatafuta biashara ya kujishikiza.

Kuna wengine ambao wanasema chuma ulete na mambo ya kishirikina yamewafanya wapate hasara kwenye biashara zao. Hawa ni wengi na ni kazi ngumu sana kuwaambia wkamba uchawi wa biashara zai upo ndani yao wenyewe.

SOMA; Kinachofanya Maisha Yawezekane Na kinachoyafanya Yawe Rahisi.

Na kuna wachache ambao wameamua kuingia kwenye biashara, wameamua hiki ndio kitu wanachotaka kufanya, wameweka malengo makubwa na wanajua juhudi na maarifa yao ni muhimu sana.

Kama upo kwenye hayo makundi ya juu ukiacha hilo la mwisho, naweza kukuambia kwamba utateseka sana kwenye biashara. Utakazana sana lakini usione kile ambacho unategemea kufanya.

Mafanikio ya biashara yako yanaanza na wewe mwenyewe, yanaanza na mtizamo sahihi juu ya biashara. Chagua biashara kuw andio maisha yako na utaona mabadiliko makubwa kwenye biashara yako.

SOMA; Fanya Kama Hakuna Anayekuangalia.

Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.

Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.