Hata uwe na bidhaa au huduma bora kiasi gani, kama watu hawajui ipo, huna biashara. Jukumu lako kubwa kwenye biashara ni kuweza kulifikia soko lako. Kila mwenye uhitaji ajue hitaji lake linaweza kutatuliwa wapi.

Njia ya uhakika ya kulifikia soko lako ni kupitia matangazo. Katika matangazo mteja anajua kwmaba upo na anajua huduma unazotoa.

Njia zilizozoeleka za kutangaza biashara kama kupitia redio, magazeti, tv na vyombo vingine vya habari ni ghali sana. Mfanyabiashara mdogo ni vigumu sana kuweza kumudu gharama hizi.

SOMA; Hawa Ndio Wateja Rahisi Kuwapata Kwenye Biashara Yako.

Lakini bado haimaanishi kwmaba huwezi kutangaza biashara yako. Leo nakushirikisha njia rahisi za kuweza kutangaza biashara yako.

1. Tumia wateja ambao tayari unao. Hawa ni wateja rahisi kuwapata na kama ukienda nao vizuri, hawa ndio watakutangazia biashara yako kwa wengi zaidi. Waridhishe wateja ulionao sasa na washawishi wawaambie wengine kuhusu biashara yako.

2. Tumia mitandao ya kijamii. Facebook na instagram ni mitandao yenye watumiaji wengi sana hapa Tanzania kwa wakati huu ninaoandika. Hakikisha unakuwa na kurasa zako katika mitandao hii na unajichanganya na wateja wako. Usitumie mitandao hii kutangaza tu, bali jichanganye na wateja wako na itakuwa rahisi kwao kununua kwako kwa sababu wanajua wewe ni mwenzao.

SOMA; Kijana Punguza Mambo Haya Ili Uweze Kupata Mtaji Wa Kuanza Biashara -1

3. Kuwa na kadi ya biashara(business card). Hii ni kadi ndogo yenye taarifa zako kuhusu biashara unayofanya na mawasiliano yako. Unaweza kumpatia mtu kadi hii na anapokuwa na shida akakutafuta.

4. Hudhuria makongamano mbalimbali ya kibiashara. Kuna makongamano mengi ya kibiashara yanayoandaliwa. Hudhuria makongamano haya na ongea na watu wnegi uwezavyo. Taja aina ya biashara unayofanya kwenye maongezi yako na wengine na unaweza kupata mtandao mzuri. Pia huu ndio wakati mzuri wa kutumia kadi yako.

5. Toa ofa. Hii pia ni njia rahisi ya kutangaz abiashara yako. Unapotoa ofa, watu wengi wataizungumzia na hii itawaleta wengi zaidi kwenye biashara yako. Kama watapata huduma nzuri, watarudi tena hata baada ya ofa kuisha.

SOMA; KITABU; Jinsi Ya Kufaidika Na Mabadiliko Yanayotokea Kwenye Maisha.

Je unatumia njia zipi kati ya hizo tano kutangaza biashara yako? Baada ya kujifunza leo utaanza kutumia njia nyingine zipi? Karibu kwenye maoni hapo chini tusirikishane ili kujifunza zaidi.

Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.

Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.

KARIBU KWENYE SEMINA YA MAFANIKIO KUPITIA BIASHARA MWAKA 2015.

AMKA CONSULTANTS imekuandalia semina ya mafanikio kwenye biashara mwaka 2015. Katika semina hii utajifunz amambo yote muhimu yatakayokuwezesha kuanza, kukuza na kufikia mafanikio kwenye biashara yako. Semina itaanza tarehe 04/05/2015 na itaendeshwa kwa mwezi mzima kwa njia ya mtandao(yaani email). Mwisho wa kujiunga na semina hii ni tarehe 01/05/2015. Wahi sasa kujiunga ili upate maarifa yatakayokuwezesha kufanikiwa kwenye biashara. Kwa maelezo zaidi na jinsi ya kujiunga bonyeza maandishi haya.