Ushauri Muhimu Kwa Waandishi Wa Blog; Idadi Sahihi Ya Wasomaji Unaohitaji Ili Kufanya Biashara.

KARIBU KWENYE SEMINA YA MAFANIKIO KUPITIA BIASHARA MWAKA 2015.

AMKA CONSULTANTS imekuandalia semina ya mafanikio kwenye biashara mwaka 2015. Katika semina hii utajifunz amambo yote muhimu yatakayokuwezesha kuanza, kukuza na kufikia mafanikio kwenye biashara yako. Semina itaanza tarehe 04/05/2015 na itaendeshwa kwa mwezi mzima kwa njia ya mtandao(yaani email). Mwisho wa kujiunga na semina hii ni tarehe 01/05/2015. Wahi sasa kujiunga ili upate maarifa yatakayokuwezesha kufanikiwa kwenye biashara. Kwa maelezo zaidi na jinsi ya kujiunga bonyeza maandishi haya.

Mwezi may mwaka 2014 tuliendesha semina ya jinsi ya kutengeneza fedha kwenye mtandao kwa kutumia blog. Hii ilikuwa semina maalumu kwa wale wote ambao wanapenda kutumia mtandao wa intaneti kutengeneza kipato. Katika semina hii tulishirikishana mengi ya muhimu ambayo mtu anatakiwa kuzingatia ili kuweza kugeuza huduma yake na kuwa biashara.

pesa mtandao

Pamoja na semina ili kupita, bado kulikuwa na hitaji kubwa la watu kutaka kujua wanawezaje kutengeneza fedha kwenye mtandao kwa kutumia blog. Hivyo tuliandaa kitabu chenye maelekezo yote kuanzia jinsi ya kufungua blog yako, uandishi mzuri wa makala na hata jinsi ya kuigeuza blog yako na kuwa biashara.(Unaweza kukipata kitabu kwa kubonyeza hapa)

Pamoja na elimu yote hii ambayo tumeshaitoa bado waandishi wengi wa blog wanashindwa kuzigeuza blog zao na kuwa biashara. Wengi wanajikuta wakikata tamaa na kuona hakuna biashara inayowezekana kupitia blog au mtandao wa intaneti.

Sasa leo nataka nikushirikishe mambo mengine muhimu sana ya kuzingatia ili kuweza kuufanya uandishi wako wa blog kuwa wa kibiashara.

Ni idadi kiasi gani unayohitaji ili uweze kutengeneza kipato kupitia blog yako?

Hapa waandishi wengi wa blog hufikiri ni idadi kubwa sana ya watu, labda watu laki moja, labda milioni. Ni kweli idadi kubwa ya wasomaji inaweza kuonesha urahisi wa kufanya biashara kupitia blog. Lakini sio kwamba ukiwa na idadi ndogo huwezi kufanya biashara, tena kwa idadi ndogo unaweza kufanya biashara vizuri kuliko kwa idadi ndogo.

Sasa basi ni idadi kiasi gani unahitaji? Kwa kuanzia, wasomaji 100 wanakutosha kuanza kutengeneza fedha kwa kutumia blog yako. Wasomaji 100? Mbona wachache, mbona tayari ninao, mbona sizioni fedha? Najua haya ndio yatakuwa maswali ya wengi. Ndio unahitaji kufikisha angalau wasomaji 100, na hawa sio wasomaji tu wanaofungua makala zako na kufunga, bali hawa ni wasomaji ambao ni mashabiki wako wakubwa sana. Hawa ni wasomaji 100 ambao wanakuamini na wapo tayari kuchukua hatua pale ambapo unawaambia wafanye hivyo. Hawa ni wasomaji ambao wanakuelewa sana na zile makala unazoandika zinawasaidia kwa kiasi kikubwa sana. Hawa ni wasomaji 100 ambao anasubiri makala zako kwa hamu sana kwa sababu wanajua kuna kitu kikubwa cha kujifunza.

Sasa tuseme kwa wasomaji hawa 100 ukaandaa kitu kizuri kwao ambacho watachangia tsh elfu tano tu kwa mwezi kwa kila msomaji, hii inakuwa ni tsh laki tano kwa mwezi. Sio kiwango kibaya cha kuanzia, na hapo ni unafanya kitu ambacho unakipenda, unawanufaisha wengine kwa maarifa na wakati huo hata wewe mwenyewe unanufaika.

Kama nahitaji wasomaji 100 tu mbona ninao na fedha sizioni?

Kama nilivyosema hapo juu, wasomaji hawa 100 sio wasomaji tu, bali ni wasomaji wanaokuamini sana. Na ili uweze kufikisha idadi hii ni lazima uwe na wasomaji wengi zaidi ya hapo labda 500 au 1000 na katika hawa 100 wanakukubali sana. Hili linachukua muda, hutaandika leo na kesho halafu mwezi ujao watu wanaanza kukujazia mahela, hapana. Unahitaji muda, watu wafanyie kazi vile ambavyo unawaandikia, waone matokeo mazuri na waendelee kukubali kazi zako na hivyo kuwa mashabiki wakubwa. Hii inaweza kuchukua angalau mwaka mmoja, wa kufanya kazi ya uhakika ambayo unajua inamsaidia mtu kutoka mahali alipo na kwenda mbele zaidi.

Pia unaweza kuwa na wasomaji hao 100, ambao ni mashabiki wako wakubwa lakini ukawa huna kitu cha kuwafanya wakuchangie kiasi hiko cha fedha kwa mwezi. Hapa unahitaji kurudi mezani na kuangalia ni nini unaweza kuwapatia na wakawa tayari kuchangia. Hili sio gumu kama unawajua vizuri hawa wasomaji wako 100.

Ni aina gani ya makala unahitaji kuandika ili kuwafikia wasomaji ambao ni mashabiki wako wakubwa?

Makala unazohitaji kuandika ni zile ambazo unajua kwa hakika zitamsaidia mtu kutoka pale alipo na kwenda mbele zaidi. Ni hivyo tu, hakuna kigezo kingine. Huandiki kuwafurahisha watu, bali unaandika kuwasaidia watu. Mtu akikuambia kwamba unaandika makala ndefu sana hivyo zinachosha kusoma, jua huyu sio msomaji unayemlenga, huyu sio mtu mwenye tatizo ambaye yupo tayari kutafuta suluhisho, huyu hawezi kuwa shabiki wako mkubwa na kuwa tayari kuchangia huduma yako japo kwa kiasi kidogo. Urefu au ufupi wa makala haijalishi kwa msomaji ambaye ni shabiki wako mkubwa, yeye anachojali ni yale maarifa anayopata kutoka kwneye makala unayoandika. Anajali zaidi kupata suluhisho la tatizo lake kuliko kujali idadi ya maneno uliyoandika.

Wakati naanza kuandika makala hizi za kusaidia watu, malalamiko makubwa ya watu yalikuwa kwamba makala unazoandika ni ndefu mno, watanzania ni wavivu wa kusoma, hawawezi kusoma makala ndefu kiasi hiko. Mwanzoni nilikuwa nakubaliana na watu hao na kuwa nafupisha makala, nilichikuja kujifunza baadae ni kwamba nilikuwa nawaacha wale mashabiki wakubwa wa kazi yangu wakiwa bado na kiu kubwa, huku wale ambao nilikuwa nawaridhisha hata hawakuwa na muda huo, bado walitafuta sababu kwa nini hawawezi kusoma makala hizo. Baadae nikajua kwmaba sijaribu kumuandikia kila mtu, namuandikia shabiki wa kazi yangu, ambaye inamsaidia, ambaye yupo tayari kusikia kutoka kwangu, ambaye yupo tayari kufanyia kazi yale ambayo nitamwambia. Kuna watu wanaweza kusoma gazeti la michezo ukurasa wa kwanza mpaka wa mwisho, mimi siwezi hivyo, kuna watu wanaweza kusoma ukurasa mzima wa gazeti la hadithi ya mapenzi bila ya kuacha, mimi siwezi hivyo. Tatizo sio urefu au ufupi wa makala, tatizo ni je huyu unayemuandikia ni shabiki wako mkubwa? Mpaka kufikia sentensi hii ninayoandika ni zaidi ya maneno 800, lakini bado wewe unasoma, kwa sababu unajua hiki unachosoma unakielewa na kitakusaidia. Wale ambao hawakukielewa waliishia aya ya kwanza au ya pili, sina tatizo nao, maana hao sio washabiki wa eneo hili. Ila wewe umejifunz ana umeondoka na kitu ambacho unaweza kukifanyia kazi na ukabadili blog yako kwa kiasi kikubwa sana.

Hayo ni mambo mawili makubwa ambayo waandishi wengi wa blog wanakosea sana, kukosa washabiki wakubwa, yaani wasomaji wachache ambao wapo tayari kukusikiliza na kujaribu kumridhisha kila mtu badala ya kutoa maudhui yenye kusaidia kwa wale wasomaji ambao wapo tayari kusikia kutoka kwako.

Mambo mengine muhimu ambayo tulijifunza kwenye kozi ile na pia tuliyasisitiz akwenye kitabu ni;

1. Kupenda kile unachoandika. Ndio unahitaji kukipenda sana ili kuweza kujifunza zaidi na kuwapatia wasomaji wako maarifa sahihi yatakayowawezesha kuboresha kile wanachofanya na maisha yao kwa ujumla. Kama unaandika kuhusu ufugaji wa kuku, basi hakikisha mtu yeyote mwenye tatizo la ufugaji wa kuku akifika kwako anapata suluhisho.

2. Andika kitu kinachoeleweka. Huandiki kumuonesha msomaji kwmaba wewe unajua maneno magumu, au unajua na kiingereza. Mwandikie msomaji wako kwa lugha rahisi sana ambayo ataielewa, na ataweza kuchukua hatua.

3. Makala zako zilenge kumsaidia msomaji. Hakuna la kuongeza hapo.

4. Kuwa na utaratibu unaoeleweka. Weka utaratibu ambao utaufuata na msomaji ataweza kuufuata na atategemea kupata kitu kutoka kwako. Usiweke makala kama ajali, yaani wiki moja unaandika kila siku, halafu unakaa wiki tatu hujaandika kabisa, unakuja tena wiki nyingine unaandika wka fujo. Hivi huwezi kutengeneza wasomaji ambao ni mashabiki wako wakubwa. Kama muda wako unakuruhusu kuandika mara moja kwa wiki fanya hivyo na mwambie msomaji wako ni siku gani ategemee kupata makala kutoka kwako na simamia hilo. Jitahidi sana hata kama una dharura kiasi gani uweze kutimiza ratiba yako. Msomaji wa AMKA MTANZANIA anajua atapata makala kila siku za wiki, jumatatu mpaka ijumaa. Msomaji wa MAKIRITA AMANI anajua atapata makala kila siku, jumatatu mpaka jumapili, na hata iwe sikukuu, kuna kitu kitakuwepo kipya cha kujifunza. Fanya hivi, utatengeneza wasomaji wanaotaka kusikia kutoka kwako.

Kuna mengi tunaweza kujadili hapa, hebu anza na hayo machache niliyokushirikisha, na kama hujapata kitabu kile cha blog kipate hapa leo hii ili uweze kuifanya blog yako kuwa biashara.(bonyeza haya maandishi kukipata)

Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya kutengeneza wasomaji ambao ni mashabiki wakubwa wa kazi zako.

TUPO PAMOJA.

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

kitabu-kava-tangazo4323

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: