Ili uweze kufanikiwa kwenye biashara, hasa kupitia masoko na mauzo basi unahitaji kuijua saikolojia hasa upande wa tabia za binadamu.
Binadamu wana tabia fulani ambazo zinawafanya wachukue maamuzi au wasichukue maamuzi katika hali fulani wanazokutana nazo. Tabia hizi ni nyingi na tutaendelea kujifunza kwenye kipengele hiki cha BIASHARA LEO kadiri siku zinavyokwenda.
Leo tutajifunza saikolojia ya kuuza. Katika saikolojia ya kuuza kuna tabia ambayo watu wengi sana wanayo. Na kwa kuijua tabia hii unaweza kuongeza mauzo yako kw akiasi kikubwa sana kwenye biashara unayofanya.
SOMA; Kitu Hiki Kimoja Ni Muhimu Kuliko Kiwango Cha Fedha Unachotaka.
Kama kwenye biashara yako unauza bidhaa au huduma za bei tofauti tofauti, anza kumuuzia mteja bidhaa ya bei kubwa kwanza kabla ya kumuuzia ya bei ndogo. Mteja anaposhawishika na akatoa bei kubwa ni rahisi sana kulipia kitu kingine cha bei ndogo. Ila unapoanza kumuuzia kitu cha bei ndogo, itakuwa vigumu sana kwake kukubali kununua cha bei kubwa.
Kwa mfano kama unauza nguo, ukiweza kumshawishi mteja akanunua suti ya laki tano, ni rahisi sana kumuuzia soksi za elfu 20. Hii ni kwa sababu akilinganisha laki tano na elfu ishirini, hii elfu 20 sio kitu. Lakini kama angekuja moja wka moja na ukajaribu kumuuzia soksi za elfu 20 angeweza hata asikusikilize.
SOMA; Fursa Zinaweza Kukupoteza…
Kama umewahi kununua kompyuta utakuwa umeliona hili mara nyingi. Baada ya kununua kompyuta ambayo bei yake ni juu labda laki tano, unaanza kuoneshwa vitu vingine vya bei ndogo ndogo, begi, flash, anti-virus, spika za nje. Vyote hivi vinakuwa vya bei ndogo ndogo elfu kumi mpaka elfu 20. Kama umeshatoa laki tano inakuwa rahisi sana kwako kutoa elfu kumi na kununua flash, hata kama huna mahitaji makubwa na flash hiyo.
Tumia mbinu hii kwenye biashara yako. Anza kumshawishi mtu anunue kitu cha bei kubwa, halafu angalia vya bei ndogo ambavyo vinaendana na kile alichonunua na mshawishi anunue, hutatumia nguvu nyingi.
Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.
Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.
KARIBU KWENYE SEMINA YA MAFANIKIO KUPITIA BIASHARA MWAKA 2015.
AMKA CONSULTANTS imekuandalia semina ya mafanikio kwenye biashara mwaka 2015. Katika semina hii utajifunz amambo yote muhimu yatakayokuwezesha kuanza, kukuza na kufikia mafanikio kwenye biashara yako. Semina itaanza tarehe 04/05/2015 na itaendeshwa kwa mwezi mzima kwa njia ya mtandao(yaani email). Mwisho wa kujiunga na semina hii ni tarehe 01/05/2015. Wahi sasa kujiunga ili upate maarifa yatakayokuwezesha kufanikiwa kwenye biashara. Kwa maelezo zaidi na jinsi ya kujiunga bonyeza maandishi haya.