Moja ya makosa ambayo wafanyabiashara wengi huwa wanayafanya na yanawagharimu ni kufikiri kwamba watu wengine hawaoni kile ambacho wanakifanya. Wanafikiri kwamba wamejifungia wkenye ulimwengu wao wenyewe na kufanya mambo yao wenyewe.
Ukweli ni kwamba kama unafanya biashara na inaonesha mafanikio makubwa, kuna watu wengi wanaiona biashara hiyo na wameshaanza kufikiria jinsi ya kuingia na kukuzidi hata wewe. Kama umeridhika na mafanikio ambayo unayapata sasa kupitia baishara yako ni kwmaba unajiandalia shimo ambalo litakufukia ukiwa mzima mzima.
SOMA; Kijana Punguza Mambo Haya Ili Uweze Kupata Mtaji Wa Kuanza Biashara -1
Kuna watu hawalali usiku na mchana wakifikiria ni jinsi gani wanakunyang’anya wateja wako. Na sio kwamba watakunyang’anya kwa nguvu, la hasha, watakunyang’anya kilaini mno. Wataangalia ni kitu gani hufanyi na wao wataanza kufanya. Wataangalia udhaifu wako na wataimarisha kwao, wataangalia ni wapi ambapo hujafikiria bado na watafikiria mbele yako.
Wkati utakapokuja kustuka kwenye usingizi mnono wa kuridhika uliokuwa umelala unakuta wenzako wameshaweka mizizi mirefu mno na wewe umeshapotezwa kabisa.
Amka sasa kabla mambo hayajawa mabaya, stuka kabla wajanja hawajakuondoa sokoni. Hakikisha wewe ndio unakuwa mjanja. Hakikisha kila mara unafikiria njia mpya za kuboresha biashara yako na kutoa huduma nzuri zaidi kwa wateja wako. Hakikisha unashindana na wewe mwenyewe kwanza ili usiridhike na kujiona upo juu sana.
SOMA; Tumia Vikwazo Ulivyonavyo Kufikia Mafanikio.
Na uzuri ni kwamba biashara yoyote, pale ilipo ina mambo mengi sana ya kuboresha. Ni mambo mangapi utakayoanza kuboresha leo kwenye biashara yako?
Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.
Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.
KARIBU KWENYE SEMINA YA MAFANIKIO KUPITIA BIASHARA MWAKA 2015.
AMKA CONSULTANTS imekuandalia semina ya mafanikio kwenye biashara mwaka 2015. Katika semina hii utajifunz amambo yote muhimu yatakayokuwezesha kuanza, kukuza na kufikia mafanikio kwenye biashara yako. Semina itaanza tarehe 04/05/2015 na itaendeshwa kwa mwezi mzima kwa njia ya mtandao(yaani email). Mwisho wa kujiunga na semina hii ni tarehe 01/05/2015. Wahi sasa kujiunga ili upate maarifa yatakayokuwezesha kufanikiwa kwenye biashara. Kwa maelezo zaidi na jinsi ya kujiunga bonyeza maandishi haya.