Unapoanza biashara, una kazi kubwa ya kufanya kujua wateja wako ni watu wa aina gani. Hili ni jambo muhimu sana ili uweze kuwapatia kile ambacho wanahitaji, uweze kutatua matatizo yao na kisha wakupatie wewe fedha.

Japokuwa wateja wako wanawez akuwa na tatizo sawa, lakini bado hawafanani. Kutokana na tabia tofauti tofauti za watu, hata wateja wako pia wanakuwa na tofauti. Wote wana tatizo sawa, na wewe una suluhisho la tatizo lao, bado sio wote watakaokuja kwa wakati mmoja kupata suluhisho hilo. Hili ni eneo muhimu sana unalotakiw akujua kuhusu biashara yako.

SOMA; Hivi Ndivyo Unavyodhulumu Maisha Yako Wewe Mwenyewe.

Kama unaanza biashara mpya, au kuna kitu kipya umeanzisha wkenye biashara yako kuna makundi matatu ya wateja.

Kundi la kwanza ni la wateja ambao ni wabunifu. Hawa ni watu ambao wanapenda kuwa wa kwanza kutumia kitu pale ambapo kinatoka. Hawa ni watu ambao wanajua ni nini wanataka na hivyo hujaribu haraka sana pale wanaposikia kuna kitu kipya kimetoka. Kundi hili lina watu wachache sana.

Kundi la pili ni la wateja ambao wanabadilika haraka. Hawa ni watu ambao tayari wanasehemu nyingine ambayo wanapata huduma unayotoa ila wanapenda kubadilika, wanakuja kujaribu huduma yako na kama itakuwa bora watakuwa tayari kufanya biashara na wewe. Kundi hili lina watu wachache pia ila hawa ni wengi kuliko kundi la kwanza.

SOMA; USHAURI; Jinsi Unavyoweza Kuondokana Na Changamoto Za Kuendesha Biashara Na Kuweza Kufikia Mafanikio Makubwa

Kundi la tatu ni la wateja ambao wanabadilika taratibu sana. Hili ndio kundi kubwa na lina watu wengi sana. Kama ilivyo tabia ya binadamu, hatupendi mabadiliko, tunapend akuendelea kufanya kile ambacho tumezoea kufanya. Kundi hili la wateja huchukua muda kidogo mpaka wawe tayari kufanya biashara na wewe. Hawa ni wale wateja ambao wanasubiri mpaka waone watu wengi wanatumia huduma yako na imewasaidia sana ndio na wao watakuwa tayari kuitumia.

Sasa unayatumiaje haya makundi matatu?

Kwanza kabisa unapoanza biashara yoyote au unapoanzisha kitu kipya, usikate tamaa mwanzo unapoona watu ni wachache kuliko ulivyotegemea. Kuna wengine wengi ambao bado wanausoma mchezo kabla hawajaingia kwenye biashara na wewe.

SOMA; Kitu Pekee Kinachoweza Kuiharibu Siku Yako Na Jinsi Unavyoweza Kuepuka…

Pili tumia vizuri makundi mawili ya mwanzo, wabunifu na wanaobadilika haraka. Wapatie huduma nzuri sana hawa kiasi kwamba watakuwa tayari kusambaz ahabari zako na hivyo kuwafikia haraka wale wanaobadilika taratibu.

Tatu endelea kuboresha biashara yako, mambo yanabadilika wka kasi sana. Ila usibadilke mpaka ukawapoteza wateja wako.

Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.

Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.

KARIBU KWENYE SEMINA YA MAFANIKIO KUPITIA BIASHARA MWAKA 2015.

AMKA CONSULTANTS imekuandalia semina ya mafanikio kwenye biashara mwaka 2015. Katika semina hii utajifunz amambo yote muhimu yatakayokuwezesha kuanza, kukuza na kufikia mafanikio kwenye biashara yako. Semina itaanza tarehe 04/05/2015 na itaendeshwa kwa mwezi mzima kwa njia ya mtandao(yaani email). Mwisho wa kujiunga na semina hii ni tarehe 01/05/2015. Wahi sasa kujiunga ili upate maarifa yatakayokuwezesha kufanikiwa kwenye biashara. Kwa maelezo zaidi na jinsi ya kujiunga bonyeza maandishi haya.