Moja ya mambo ambayo yanaulizwa sana na watu wengi wanaowasiliana na mimi kwa ajili ya ushauri ni kuhusu kuingia kwenye biashara nyingine. Yaani unakuta mtu anafanya biashara ya aina fulani na sasa anataka kuingia kwenye biashara ya aina nyingine. Watu wengi huanza kupata mawazo ya aina hii pale wanapoona biashara wanayofanya sasa ina changamoto nyingi au ile biashara wanayotaka kuiendea inaonekana kulipa kuliko biashara wanayofanya sasa. Kuhama kwenye biashara moja na kwenda kwenye biashara nyingine ni jambo ambalo linahitaji umakini mkubwa sana. Kama utashindwa kuwa makini unaweza kujikuta kwenye matatizo makubwa kuliko hata uliyofikiri unayo mwanzoni.
Katika makala hii ya leo tutaangalia mambo unayotakiwa kuzingatia kabla hujafanya maamuzi ya kuacha biashara unayofanya sas ana kuingia kwenye biashara nyingine. Mambo hayo ni kama ifuatavyo;
1. Jua sababu hasa yaw ewe kufikiria kuhama biashara.
Katika jambo lolote ambalo mtu anafanya, kuna sababu ambazo zinamsukuma kufanya au zinamvuta kufanya. Sababu zinazosukuma ni zile changamoto ambazo unakuwa nazo wkenye biashara unayofanya sasa. Na sababu zinazovuta ni yale mazuri unayoyaona kwenye biashara nyingine na unashawishika kuingia wkenye biashara hiyo. Sasa wewe unatakiwa kwenda zaidi ya hapo, kama biashara unayofanya sasa imekuwa na changamoto, je changamoto hizo zinatokana na nini? Je umechukua hatua gani ili kupambana na changamoto hizo? Je umeshajaribu kila njia inayowezekana kupambana na changamoto hizo?
Kama biashara unayotaka kuingia inaonekana kuw anzuri kuliko unayofanya sasa, je uzuri wake unatokana na nini? Je uzuri unaouona sas andivyo biashara ilivyo au ni wakati huu tu ambapo msimu unaweza kuwa mzuri wka biashara hiyo? Je ni watu wangapi wameiona biashara hiyo kama wewe na wanataka kuingia humo? Kwa kujiuliza maswali haya ya ndani kutakufanya ufikiri kwa kina zaidi na hivyo kufanya mamauzi ambayo ni mazuri kwako na kwa biashara yako. Kushindwa kujiuliza na kujipa majibu ya maswali hayo muhimu kutakufanya uchukue maamuzi ambayo sio mazuri na kukuingiza kwenye matatizo makubwa.
2. Biashara unayoifanya sasa umeshafikia kileleni.
Jambo la pili na la kuzingatia ni kuhusu biashara unayofanya sasa. Umeshajiuliza kwenye maswali muhimu hapo juu ila hapa utaangalia biashara yako ilipofikia na pale ambapo ingeweza kufikia. Usifikirie kuingia wkenye biashara nyingine kama bado hujaifikisha biashara uliyonayo sasa kwenye kilele. Kilele ninachozungumzia hapa ni ule ukuaji wa juu kabisa wa biashara ambapo umeshalifikia soko lote la biashara yako. Kama tayari umeshamfikia kila ambaye anaweza kuwa mteja wako na kutengeneza soko jingine itakuwa changamoto kubwa zaidi ndio unaweza kuingia kwenye biashara nyingine. Ila kama kuna soko ambalo bado hujalifikia, weka nguvu zako kufikia soko hilo kwanza.
3. Muda wa kujifunza kuhusu biashara hiyo mpya.
Kufanya biashara fulani kwa mafanikio, haimaanishi wkmaba tayari wewe umekuw amtaalamu wa kila biashara. Katika kila biashara mpya utakayoingia kuna mambo mengi ambayo utatakiwa kujifunza. Kabla hujaingia wkenye biashara mpya, angalia mambo unayohitaji kujifunz akwneye biashara hiyo na muda utakaokuchukua mpaka na wewe uwe umebobea. Kama utahitaji muda mrefu wa kujifunza ili uwe umebobea kwenye biashara hiyo, fikiri tena kabla ya kuamua kuingia wkenye biashara hiyo. Kwenda kuanza mwanzo kabisa kwenye biashara ambayo ni mpya kunaweza kukuchosha sana na wakati mwingine kukukatisha tama.
4. Zijue changamoto za biashara unayotaka kwenda kufanya.
Hakuna biashara ambayo haina changamoto, hakuna. Lakini unapokuwa kwenye biashara moja, ambayo nayo ina changamoto, ni rahisi kuona mazuri ya baishara nyingine na sio changamoto zake. Unaweza kushawishika kwamba biashara unayokwenda kufanya ni biashara bora kuliko unayofanya sasa, ila kama hutafanya utafiti wako kwa kina unaweza ukajikuta unaingia kwenye matatizo makubwa kuliko ambayo unayakimbia.
Kuacha biashara moja na kwenda kwenye biashara nyingine ni jambo linalohitaji umakini mkubwa kabla ya kufanya. Hakikisha umeshaifanya biashara hiyo na kutumia fursa zote zinazopatikana na pia hakikisha unaijua vizuri biashara unayokwenda kufanya kabla hujaingia.
Nakutakia kila la kheri katika biashara yako.
TUPO PAMOJA.