Kila mfanyabiashara anayo malengo na mipango yake kwenye biashara anayofanya. Lakini ni wachache sana ambao wanaweza kufikia mipango yako na kuvuna matunda mazuri.
Wafanyabiashara wengi huwa na mipango mizuri ila unapofika wakati wa utekelezaji ndio ugumu unaopoonekana. Hapa ndipo mtu anaona kama haiwezekani na kuamua kurudi nyume na kuendele akufanya kile ambacho amezoea kufanya.
SOMA; Jambo Moja Muhimu Unalotakiwa Kujua Kuhusu Miasha Na Kulitumia Kila Siku Ili Kufanikiwa.
Kitu kinachosababisha yote haya ni kutokuchanganua vizuri malengo na mipango unayojiwekea. Unasema tu kwmaba unataka uongeze faida mara mbili, au unataka kukuz amtaji au unataka kuongeza wateja. Kila mtu anaweza kusema hivi, lakini mfanyabiashara aliye makini atakaa chini na kuchanganua vizuri hili. Ndio nataka kuongeza faida mara mbili, je sasa napata faida kiasi gani, na faid ayangu kubwa inatoka wapi na ni kitu gani kidogo naweza kufanya kila siku ila kikaleta mabadiliko makubw akwenye biashara yangu?
Kadiri unavyojiuliza maswali yanayohusiana na kile unachotaka, ndivyo unavyopata njia nyingi zaidi. Wewe anza na njia ambayo ni rahisi sana na huwezi kuiacha, halafu endelea kuongeza kadiri siku zinavyokwenda.
SOMA; Ugumu Wa Mwanzo Mgumu…
Biashara yako haitakuwa kwa maneno tu, biashara yako haitakuwa mipango mizuri, biashara yako itakua kw akile unachofanya na kikaleta mabadiliko kwenye biashara yako. Changanua vizuri malengo na mipango yako na ifanyie kazi mara moja.
Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.
Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.