Katika wakati wowote na popote ulipo ni lazima uweze kuielezea biashara unaofanya kwa sentensi moja. Ni lazima ndani ya dakika moja uweze kumweleza ni biashara ya aina gani unayofanya na inaelekea wapi, au ina mahitaji gani. Ukishindwa kufanya hivi basi hua biashara.

Huna biashara kwa sababu huijui biashara yako vizuri na kama huijui biashara yako vizuri unajipa nafasi kubwa ya kutengeneza ushindani ambao utakuondoa kwenye biashara hiyo.

SOMA; Huyu Ni Mjasiriamali Mwenye Hamasa Kubwa sana. Unaweza kujifunza kila kitu kutoka kwake.

Njia nyingine rahisi ya kujipima kama unaijua biashara yako ni kama unaweza kumweleza bibi yako wa miaka 80 ni biashara gani unafanya na akakuelewa. Au mtoto wa darasa la tano, unaweza kumwambia ni biashara gani unafanya na akakuelewa.

Unaweza kuona kama haya ni mambo yasiyo na maana ninayokuambia hapa, ila yana msingi sana. Kama huwezi kuielezea biashara yako kwa watu ambao hata hawahusiki na biashara hiyo na wakaielewa, unapoteza wateja wengi sana. Jinsi ambavyo inakuwa rahis kuwambia watu biashara yako, ndivyo inavyokuwa rahisi kwao kuwaambia wengine na hivyo kukuletea wateja wengi zaidi.

Kwa mfano kama unafanya biashara ya kuandaa na kuuza software za kufanya mahesabu ya biashara, badala ya kuanza kumwambia mtu kwamba unatengeza software yenye uwezo mkubwa wa kuandaa data na mahesabu ya biashara, mwambie unafanya biashara ya kusaidia wafanyabiashara kuandaa mahesabu yao kwa usahihi na urahisi.

SOMA; Kauli Mbili Za Kuacha Kutumia Leo, Maana Zinaashiria Kushindwa.

Eleza biashara yako kwa lugha rahisi na inayoeleweka, huna haja ya kuweka maneno magumu ya kibiashara, kikubwa ni mtu aelewe unafanya nini, unatatua tatizo gani na atakapokutana na mwenye tatizo atamwelekeza kwako.

Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.

Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.