Unaweza kuw ana biashara nzuri sana, una bidhaa au huduma bora kabisa inayoweza kutatua matatizo ya mtu na kuboresha maisha yake. Ila kila unapomwambia mtu kuhusu biashara yako, au unapowatangazia watu ambao unaona wanafaa kuwa wateja wako, hawaonekani kuwa tayari kununua bidhaa au huduma hiyo.

Katika hali kama hii ni rahisi kukata tamaa na kuona labda bidhaa au huduma yako haina soko. Unaweza kuwa sahihi kufikiri hivyo ila pia unaweza kuwa haupo sahihi.

SOMA; Hatua Saba (7) Za Kuweka Malengo Na Kuweza Kutimiza Ndoto Zako.

Kabla hujakubali kwmaba bidhaa au huduma yako haina soko, hakikisha umetafuta watu ambao wana maumivu na kuona kama hawatakuw atayari kutumia bidhaa au huduma yako. Watu wenye maumivu ni wale watu ambao wanatatizo kubwa ambalo ni lazima walitatue na biashara yako inawez akutatua tatizo hilo.

Hakuna mtu anayeweza kuishi na maumivu kila siku, lazima atatafuta njia ya kuondokana na maumivu hayo. Sasa hili ndio lengo lako kwneye biashara, kutafuta watu ambao wana matatizo ambayo hawawezi kuendelea kuishi nayo na wewe unawapatia suluhisho.

SOMA; Sababu Kumi(10) Kwa Nini Uendelee Kubaki Kwenye Ajira Kwa Muda Kabla Ya Kujitosa Moja Kwa Moja Kwenye Ujasiriamali.

Kwa njia hii utawapata wateja wako, na kama hutapata mwenye maumivu ya kweli basi unaweza kuangalia ni jinsi gani unaweza kubadili biashara yako ili iweze kutatua tatizo linalowasumbua wengi.

Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.

Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.