Watu wengi wamekuwa wakiniandikia kwamba wanataka kuanza biashara ila bado hawajawa tayari. Wanakuwa na sababu nyingi ambazo huzitumia na hufikiria wakimaliza mambo fulani kwanza ndio wataingia kwenye biashara.

Sasa kama na wewe ni mmoja wa watu ambao wanafikiria kwamba bado hawajawa tayari kuingia kwenye biashara, nataka nikuambie kitu kimoja, hakuna siku utakayokuwa tayari. Kama haupo tayari kuingia kwneye biashara leo, hakuna siku utakayokuwa tayari. Labda kama hujafikiria kuingia kwenye biashara, ila kama umeshafikiria na ukaona haupo tayari maana yake hautakuwa tayari.

SOMA; Nguvu Haipo Nje, Nguvu Unayo Ndani Yako…

Sababu yoyote unayotumia leo kuchelewa kuingia wkenye biashara itaendelea kukaribisha sababu nyingine. Kama leo unasema huna mtaji, ni vigumu sana kufika siku ukasema tayari una mtaji. Kila ukipata fedha utaona bado haitoshi kuanzisha biashara. Kama unaona huna wazo zuri la biashara, kila wazo litakalokujia halitakuwa zuri na hivyo utaendelea kusubiri.

Ufanye nini sasa?

Kama kweli unataka kuingia wkenye biashara ingia sasa, tafuta watu ambao wana matatizo na unaweza kuwasaidia kwa kile unachoweza kukifanya. Anza kutoa huduma au bidhaa zako kwa watu watakaokuw atayari kukulipa. Endelea kukua kwa kuongeza wateja zaidi na kuboresha bidhaa/huduma zaidi.  Hivi ndivyo biashara inavyoanza na kukua. Ndio itakuchukua muda, lakini utajifunza mengi na utafikia mafanikio.

SOMA; Sifa Sita(6) Unazohitaji Ili Kuwa Mjasiriamali Bora.

Kama unaendele akupata changamoto kwenye biashara yako, tuwasiliane kwa namba hizo japo chini.

Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.

Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.