Unapojaribu kuwa kila kitu kwa kila mtu biashara yako inakosa maana na unashindwa kuwa chochote kwa yeyote.

Ufanye nini basi; kuna wa pekee kwa kundi fulani la watu. Usitake kumpata kila mteja aliyepo hapa duniani, bali lenga kuwapata wale watu ambao utaongeza maana kwenye maisha yao, utatatua matatizo yao na kuboresha maisha yao.

SOMA; Fanya Tukio Hili La Kihistoria Ambalo Litakupa Uhuru Uliopoteza.

Unapojaribu kufanya biashara ambayo kila mtu anaifanya, na kwa njia ile ile ambayo kila mtu anaitumia, biashara yako inakosa maana. Kama mtu anaweza kununua kwa watu wengine kumi wanaofanyabiashara kama unayofanya wewe, kwa nini anunue kwako.

Kama unataka biashara yako iwe na maana unahitaji kufanya mambo yafuatayo;

1. Jua wateja wako ni watu gani, jua matatizo yao na biashara yako inayatatuaje. Kama hujui kitu hiki muhimu ni bora usiingie kwenye biashara, manaa utapoteza muda wako bure.

2. Kuwa mbunifu na boresha kila siku. Kwanza usifanye kile ambacho kila mtu anafanya. Pili boresha kila siku kile ambacho unafanya. Usikubali kufanya kwa mazoea, kama unachofanya ni bora na kinaleta faida, watu wengi watajaribu kuiga na hivyo utakuwa unafanya kile ambacho kila mtu anafanya. Boresha zaidi na zaidi na kila siku hakikisha kuna kitu kipya unafanya kwenye biashara yako.

SOMA; Hakuna Anayejali Maisha Yako Zaidi Yako Mwenyewe.

Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.

Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.