Hivi Ndivyo Unavyoweza Kukabiliana Na Uzushi Unaojitokeza Dhidi Yako.

Linapokuja suala la uvumi na umbeya inaonekana ni kama haki kwa kila mtu. Hii ni kwa vile, mwanzoni, hilo huonekana ni suala linalowaandama watu wengine tu, hadi pale inapofikia zamu yake mtu kutetwa na kuvumishwa habari fulani mbaya dhidi yake, ndipo hasa hali inapobadilika.

Hebu tuchukulie kwamba, umeingia mahali ambapo unavumishwa au kuna umbea ambao unasemwa dhidi yako, unadhani ni njia zipi nzuri za kufanya? Jambo la maana, kwa mujibu wa ninavyofahamu ni kujaribu kuelewa unakotoka umbea au uvumi huo na sababu zake.
Kama utaweza kuchunguza nani alianzisha uvumi huo utagundua mengi, kwani ni hapo ambapo wengi huanza kujitoa kwa kusema, ‘si mimi niliyeanza! Alinieleza Christina! Na mengine mengi tu ya aina kama hiyo.
Je, uvumi huo ulikuwa na lengo la kukuudhi, ama ilikuwa ni njia ya kupotosha ukweli tu? je, Kuna mtu aliyejaribu kulazimisha jambo fulani kwako? Ama kuna mtu ana lengo la kuwafanya watu wakuchukie tu wewe bila sababu yeyote ile?
Ni muhimu kupata taarifa hii kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kuhusiana na uvumi huu, ili uweze kuwa na mawazo mazuri zaidi ya kuushughulikia na kwenda vizuri na watu wanaousambaza.
Mpate mmoja wa kati ili kupata pa kuanzia.  Unaye mtu wa unayemwamini kwenye uwanja huo wa vita? Mtambue mtu ambaye una uhakika siye aliyeanzisha uvumi huo na mvute upande wako . Mshawishi awe upande wako, na awaeleze watu wengine walio kwenye kundi hilo kwamba uvumi huo hauna kweli na cha muhimu zaidi umwambie jinsi uvumi huo unavyokuudhi.
 

Haya yanaweza kuwa mambo makubwa sana kumwomba mtu mmoja hivyo waweza kuwafuata watu wawili kukufanyia kazi hiyo, ama kumwomba mmoja wa marafiki zako kumsaidia katika kufanya kazi hiyo. Usikubali msukumo wa kiugomvi. Ni rahisi kuzama katika hasira hasa pale watu wanapokuwa wabaya kwetu.
Lakini kama ilivyo kwa aina nyingine ya misukumo ya kiugomvi, mambo huwa mabaya zaidi ikiwa tutakubali kuwapa zawadi kwa kuwaonyesha wazi kuwa tumekasirika.
Lazima ukumbuke kwamba mtu anapozusha jambo lenye lengo la kumuudhi mtu mwingine, mara nyingi hufanya hivyo kutokana na kutokujiamini ama kukosa furaha. Hii ni kweli hasa kwa watu wanaopenda kufanya hivyo kila wakati, ama kwa maneno mengine, ni watu wanaopenda kuwaudhi watu wengine ili kujifariji.
Pingana na msukumo wa kukutaka ulipe kisasi. Umekuwa muathirika wa uvumi na umbeya kila wakati  na unajua nani anayeusambaza dhidi yako, huenda ukawa na hamu ya kupambana naye ‘uso kwa uso’. Ni rahisi kuvutika nawe kuweza kutunga uongo ama kuamua kuibua hadharani siri unazozijua za mtu huyo.
Mara nyingi kulipa kisasi kwa njia hii kwa waweza kuonekana kama faraja kwako, lakini ni kwa muda mfupi tu. Mwishowe kutasaidia uvumi huo kuendelea kuranda mitaani na kukufanya uwe na msukumo wa kuendeleza uvumi huo na hivyo kutokuwa na tofauti na yule aliyeanzisha uvumi huo dhidi yako.
Punguza uwezekano wa hilo kukutokea tena. Fikiria kile unachojifunza kutokana na uvumi  fulani na acha ikusaidie kuhakikisha kwamba hiyo haitoki tena. Sasa unawezaje kukabiliana na uzushi? Mambo ya kuweza kufanya ni kama haya:-
Kuwa mwangalifu na siri zako. Kadri unavyokubali kutoa hadharani mambo yako binafsi, ndivyo wambeya wanavyopata silaha zaidi za kukushambulia, hivyo kuwa mwangalifu ni wakati gani unafichua siri zako.
Jaribu pia kutumia mfumo wa udugu. Inasaidia ikiwa utakuwa na rafiki wa karibu unayemwamini kuwa upande wako na kukusaidia wakati utakapohitaji. Muombe rafiki yako huyo achunguze kuhusu uvumi unaokuhusu na atafute ni nani anayesambaza uvumi huo.
Njia bora zaidi ya kuhakikisha rafiki yako anaendelea kuwa mwaminifu kwako ni kuchukua hatua kama hiyo kwake na kutomsaliti wakati yeye anapokuwa mlengwa wa uvumi.
Jitahidi usisambaze uvumi wa wengine. Bila shaka umewahi kusikia msemo ‘anapenda kutania lakini hajui kutaniwa’? Kwa maneno mengine, usiwe mtu anayependa kusambaza uvumi kuhusu watu wengine.
Lakini, jambo muhimu kuliko yote ni kujua kwamba, uvumi hata ungekuwa wa namna gani, hatimaye , bado utabaki kuwa uvumi, nawe utabaki kuwa wewe.
Huwa tunatakiwa kujilinda na uvumi kwani kuna wakati unaweza kutuharibia shughuli zetu, lakini hatuna haja ya kuwachukia wanaotuzushia. Kama nilivyosema, nao wana matatizo, ndiyo maana wanatuzushia, ili wajisikie vizuri.
Kwa makala nyigine nzuri hakikisha unatembelea DIRAYA MAFANIKIO kwa elimu na maarifa bora yatakayoboresha maisha yako.
Tunakutakia kila la kheri katika safari yako ya mafanikio, endelea kutembelea AMKA MTANZANIA kujifunza zaidi kila siku.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,

IMANI NGWANGWALU,

0713 048035,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s