Unapokuwa kwenye biashara, ni rahisi sana kudanganya ili tu mteja aweze kununua. Hali hii hutokea pale ambapo unahitaji sana kuuza na hivyo kuhakikisha mteja haondoki bila ya kununua. Unaweza kuona hili ni sahihi kwako kwa sababu, baada ya kudanganya utauza, ila kwa mwendo mrefu unaharibu biashara yako.

SOMA; Makundi Matatu (3) Ambayo Hayawezi Kufikia Mafanikio.

Kama ambavyo tumekuwa tunajadili hapa mara nyingi, biashara za zama hizi zinajengwa kwneye misingi ya kuaminiana. Mteja anakuchukulia wewe kama mtu ambaye unajali kuhusu matatizo na changamoto zake na ndio maana unampatia suluhisho. Sasa inapotokea ukaanza kudanganya wateja wako, unatengeneza shimo ambalo utazika biashara yako.

Ubaya wa kudanganya ni kwamba, utalazimika kuendele akutumia uongo kila mara ili usionekane tofauti. Na ubaya wa uongo ni kwmaba kuna siku mambo yote yatakuwa hadharani. Na hii itaharibu sana picha yako kwa jamii kama mfanyabiashara.

SOMA; Huu Ndio Ukweli Kuhusu Wewe.

Sema ukweli mara zote, hata kama ukweli huo utamfanya mteja asinunue, atakuheshimu na utapata wateja wazuria ambao wataendana na ukweli wako.

Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.

Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.