CONSULTANTS, naamini unaendelea vizuri na harakati zako
za kuboresha maisha yako na kufikia mafanikio makubwa. AMKA CONSULTANTS ipo
pamoja na wewe kwenye safari hii ya kuboresha maisha yako na inakupatia maarifa
na ushauri muhimu utakaokusaidia kwenye safari hii.
Kwa kuwa lengo letu AMKA CONSULTANTS ni kukuwezesha wewe kufikia
ule uwezo mkubwa ulio ndani yako, kila mara tunaangalia njia bora ya kukuwezesha
wewe kufikia uwezo huu mkubwa sana. Tunajua kwamba wewe hufanani na mtu
mwingine, licha ya kudanganywa hivi kwa muda mrefu. Hivyo tunafanya kila
linalowezekana ili kukupatia wewe maarifa na ushauri utakaokuwezesha kutumia
uwezo wako na mazingira yako kuboresha maisha yako.
Ili kuhakikisha unapata kilicho bora, kuna mabadiliko makubwa
yatakayofanyika kwenye baadhi ya blog za AMKA CONSULTANTS. Mabadiliko haya ni
kwa ajili ya kuboresha zaidi ili iwe rahisi kwako kufikia kile unachotaka
kufikia kwenye maisha yako.
Yafuatayo ni mabadiliko yatakayofanyika mapema.
KISIMA CHA MAARIFA,
Kisima cha maarifa ni blog ya kulipia inayoendeshwa na AMKA
CONSULTANTS. Blog hii ina makala nyingi sana na nzuri zinazokupatia wewe maarifa
ya biashara, mafanikio na hata uchambuzi wa vitabu. Blog hii ilikuwa na
uanachama wa aina tatu, BRONZE(tsh elfu 10), SILVER(tsh elfu 30) na GOLD(tsh
elfu50).
Kwa sasa kutakuwa na mabadiliko yafuatayo.
Kutakuwa na makala moja kwa kila siku ya juma. Jumatatu makala
ya biashara/ujasiriamali, Jumanne makala ya tabia za mafanikio, jumatano makala
ya world class, alhamisi makala ya uchambuzi wa vitabu na ijumaa makala ya
uongozi na usimamizi. Kipengele cha uongozi na usimamizi kimeongezwa ili kuweza
kukujenga wewe kuwa kiongozi bora na hata msimamizi mzuri pia. Unapokuwa kwenye
biashara, unahitaji kuwa kiongozi na wakati huo huo kuwa msimamizi. Utajifunza
yote haya kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Makala za uchambuzi wa vitabu hazitakuwa
tena kama zamani ambapo kitabu kimoja kilikuwa kinachambuliwa kwa muda, bali
kila wiki kitachambuliwa kitabu kimoja. Hii itakuwezesha wewe kujifunza mambo
mengi zaidi ya kukuwezesha kufikia mafanikio makubwa.
Kwenye makundi ya uanachama kutakuwa na mabadiliko pia. Kundi la
BRONZE litaondoka na hivyo tutabaki na SILVER ambapo ada yake ni tsh elfu 30 kwa
mwaka na GOLD ambapo ada yake ni tsh elfu 50 kwa mwaka. Waliopo kwenye GOLD
wataendelea kupata nafasi ya kuwa kwenye kundi la wasap. Wanachama wa bronze wa
sasa wataingia kwenye silver bila ya kuongeza kiwango kingine cha fedha. Lakini
wakati w akufanya malipo mapya watalipia kwa ada ya silver au gold kama
watapenda. Usikose nafasi hii nzuri ya kujifunza. Kama bado hujajiunga na KISIMA
CHA MAARIFA bonyeza maandishi haya.
Pia kuna kundi moja litaongezeka ambalo litakuwa ni PLATNUM.
Kundi hili ni la watu wachache ambao watahitaji kufuatiliwa kwa karibu sana kwa
kile wanachofanya ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea. Kundi hili
linahitaji mtu aliyejitoa kweli na yupo tayari kwenda hatua ya ziada ili kupata
kile anachotaka. Gharama za kuwa kwenye kundi hili ni kubwa na zinatofautiana
kulingana na mahitaji ya mtu. Kama utahitaji kuwepo kwenye kundi hili
tuwasiliane.
EMAIL LIST.
Mpaka kufikia sasa tuna watu elfu mbili waliojiunga na email
list ya AMKA CONSULTANTS. Watu hawa wamekuwa wanatumiwa email tatu kwa wiki na
email hizi zimekuwa zinatokana na makala zinazowekwa kwenye AMKA MTANZANIA.
Lakini ni sehemu ndogo sana ya watu walioweka email zao wanafungua email
zinazotumwa. Na sisi tunaingia gharama kutuma email hizi. Hivyo hatua ya kwanza
kabisa ni kufuta email zote ambazo hazijafunguliwa kwa zaidi ya mwezi mmoja.
Kama tungu mwezi wa nne umetumiwa email ila hujaifungua utafutwa. Tunataka
tubaki na watu wenye kiu kweli ya kujifunza ili tuweze kwenda pamoja.
Kutakuwa na mabadiliko kwenye email zinazotumwa, kwanza
hazitatumwa mara tatu kwa wiki kama ilivyokuwa mwanzo, sasa zitatumwa mara mbili
kwa wiki, jumanne na alhamisi. Labda kama kutakuwa na jambo muhimu ndio kutakuwa
na email zaidi ya hapo kwa wiki. Email zitakazotumwa sasa sio za makala iliyopo
kwenye blog, bali yatakuwa mazungumzo ya moja kw amoja kutoka kwangu kuja kwako.
Nitakuwa nakushirikisha mambo mbalimbali ambayo naona yanaweza kukusaidia sana.
Na mwisho nitakuwekea link ya makala zilizopo kwenye blog.
Nitakuwa natoa mafunzo makubwa sana kupitia email nitakazokuwa
natuma na yatakuwa na thamani kubwa sana. Ungehitaji kulipia gharama kiasi
kupata mafunzo haya, lakini gharama yako itakuwa ni kufungua email na kusoma kwa
wakati. Ukishindwa kufungua email kumi kwa mfululizo, moja kwa moja unaondoka
kwenye mfumo wetu wa email. Na sio sisi tunakuondoa bali ni mfumo unakuondoa
wenyewe kwa jinsi tulivyouweka.
Hivyo fungua email yako kila siku ya jumanne na alhamisi uweze
kujifunza. Kama bado hujajiunga na mfumo huu wa email bonyeza maandishi haya.
AMKA TV.
Kwa sasa utakuwa unapata video mbalimbali za mafunzo na
kuhamasisha kupitia mtandao wa YOUTUBE. Video hizi zitakuwa kwneye channel
inayoitwa AMKA TV. Bado tunaifanyia kazi chanel hii ili kuweza kukuleta mafunzo
bora zaidi kwa sasa tunaanza na video za kutengeneza wenyewe ila baadae tutakuwa
tunafanya mahojiano na watu mbalimbali ambapo utajifunza mambo mengi na mazuri.
Ingia kwenye channel ya AMKA TV kwa kubonyeza maandishi haya na hakikisha
unasunscribe(kujiunga) nayo ili ufahamishwe kila video mpya
inapowekwa.
Makala kwenye AMKA MTANZANIA na JIONGEZE UFAHAMU zitaendelea
kuwepo kila siku ya juma na kwa utaratibu uliopo sasa. Kuna vitu vingine vizuri
bado tunavifanyia kazi na vitakapokuwa tayari tutawashirikisha. Lengo ni wewe
uweze kufikia malengo na mipango uliyojiwekea kwenye maisha yako.
Nakukaribisha sana kwenye AMKA CONSULTANTS, karibu ujifunze na
uhamasike ili uweze kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako.
TUPO PAMOJA.
Makirita Amani,
