Biashara ni uaminifu, kama hakuna uaminifu hakuna biashara. Kama bado unafanya biashara kwa mazoea yale ya zamani kwamba biashara ni kuwaibia watu, usiendelee kusoma makala hii maana tutakavyojadili hapa hutavielewa. Badala yake fungua makala za nyuma kwenye kipengele hiki cha BIASHARA LEO na uanze kujifunza yale muhimu kwanza.
Sasa twende pamoja kwa wale ambao wanafanya biashara kwa kujenga mahusiano mazuri na wateja kama ambavyo tumekuwa tukijadili mara kwa mara. Uaminifu kwa wateja wako ni muhimu sana. Wateja wanapokuamini wanafanya biashara na wewe kwa muda mrefu na watawaambia wengine kuhusu wewe.
Hata pale ambapo utafanya mabadiliko ya bei kwenye biashara yako, kama wateja wanakuamini hawatasumbuka na hilo, na wataendelea kufanya biashara na wewe.
SOMA; Hii Ni Kazi Yenye Malipo Makubwa Sana Ambayo Unaweza Kujifunza Kuifanya
Unawezaje kujenga uaminifu kwa wateja wako? Yaani ufanye nini ili wateja wako wakuamini na waendelee kufanya biashara na wewe? Ni rahisi, fanya mambo haya;
1. Waheshimu wateja wote bila ya kujali ni kiasi gani wanachangia kwenye biashara yako.
2. Wasikilize wateja wako kwa kile wanachosema na jibu maswali yao.
3. Onesha kujali kwa hali wanazopitia.
4. Kuwa mkweli hata kama itapelekea wao kutonunua kwako.
5. Kutoa mawazo na ushauri kwa wateja wako bure.
6. Kufanya kile ambacho umeahidi utafanya.
7. Kuwafanya wateja wako wajue kama utashindwa kufanya kile ulichoahidi kufanya.
8. Kujali muda wako na wa wateja wako pia.
9. Kutokuwa na tamaa kwenye biashara yako.
10. Kufanya kila kilicho bora katika biashara yako.
Anza na hayo machache na utaona mabadiliko makubwa kwneye biashara yako.
Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.
Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.
Jiunge na COACHING/MENTORSHIP PROGRAM ambapo utapata muongozo wa hatua kwa hatua mpaka ufikie mafanikio kwenye kazi au biashara unayofanya. Bonyeza haya maandishi kupata maelekezo ya programu hii.