Katika biashara kuna mitazamo miwili mikubwa, mtazamo wa kwanza ni wa kuvuna, na mtazamo wa pili ni wa kujenga.

Mtazamo wa kuvuna.

Hapa ni pale ambapo mfanyabiashara anaangalia ni kitu gani anakipata sasa. Yeye anafikiria kuvuna tu na hivyo anapoipata fursa anaitumia kwa uhakika. Na kama hakuna njia ya kuvuna anahama na kwenda kwenye biashara nyingine. Katika aina hii ya mtazamo mfanyabiashara anakuwa tayari kutoza gharama kubwa sana ili mradi tu afikie lengo lake. Anakuwa hana mpango wa kukaa kwenye biashara hiyo kwa miaka mingi na hivyo kuhakikisha anavuna haraka kabla mavuno hayajaisha.

SOMA; Kama Unataka Kumaliza Matatizo Yako Ya Fedha Fanya Kitu Hiki Kimoja.

Mtazamo wa kujenga.

Hapa ni pale ambapo mfanyabiashara anaangalia ni jinsi gani anaweza kujenga ili baadae aweze kunufaika zaidi. Mfanyabiashara anafikiria zaidi kujenga mtandao wa watu wanaomuamini na watakaofanya naye biashara kwa muda mrefu. Haangalii kuvuna haraka na kuondoka. Hata kwenye upande wa bei anaweka bei ndogo ambayo watu wataimudu na kuendelea kuwa naye kwa muda mrefu. Mtazamo huu wa kujenga unamfanya mfanyabiashara kunufaika kwa muda mrefu sana na huku akijijengea mtandao mkubwa wa watu wanaomuamini.

Je wewe unaendesha biashara yako kwa mtazamo gani? Mtazamo wa kuvuna utakupatia faida kwa muda mfupi ila utakuzuia kufaidika kwa muda mrefu na kila wakati itakuwa ni kama unaanza biashara. Mtazamo wa kujenga utakupatia faida kidogo ila faida hii utaipata kwa muda mrefu na kadiri muda unavyokwenda inaendelea kuongezeka. Kama utachagua mtazamo wa kujenga, utajihakikishia kufanikiwa kwenye biashara yako.

Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.

Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.

Jiunge na COACHING/MENTORSHIP PROGRAM ambapo utapata muongozo wa hatua kwa hatua mpaka ufikie mafanikio kwenye kazi au biashara unayofanya. Bonyeza haya maandishi kupata maelekezo ya programu hii.