Ni jambo la kushangaza kwenye maisha kwamba baadhi yetu tunaishi
maisha ambao hata hatuyajui. Tunatumia muda wetu mwingi kuishi maisha ambayo
hata hatukupanga kuyaishi. Tunajikuta tunaishi maisha tofauti kabisa kwa sababu
tunalazimika kuishi maisha ambao kila mtu anaishi.

Tumeshazungumza sana kuhusu kuishi maisha ya wengine, leo ngoja
tuzungumze kufanya kazi za wengine.

Kama imetokea kazi unayoifanya ikawa ndio kitu unachopenda
kufanya upo kwenye nafasi nzuri sana. Na mafanikio yapo mbele yako. Ila ni nadra
sana kuwa kwenye kundi hili ambalo lina watu wachache, asilimia 3 tu ya watu
kwenye jamii.

Kama upo kwenye asilimia 97 iliyobaki, maana yake unafanya kazi
unayofanya kwa sababu tu ndio unayotegemewa kufanya. Unafanya kwa sababu
unafikiri ndio njia pekee ya kukupatia wewe kipato. Na kila mtu ameshakuaminisha
hivyo na huwezi kuona nafasi ya kuondoka kwenye hilo.

SOMA; Mambo 20 Niliyojifunza Kwenye Kitabu Kinaitwa SELF-IMPROVEMENT
101.


Kama unafanya kile ambacho kila mtu anakutegemea ufanye, leo
nataka nikupe mbinu ya kuanza kufanya kile ambacho unapenda kufanya.

Kwanza kabisa jua ni kitu gani unapenda, licha ya kazi ambayo
sasa unaifanya. Amua ni kipi unapenda kukifanya na kila ukikifanya unajisikia
vizuri sana. Iwe ni sanaa, iwe ni kitu cha kuwasaidia wengine, iwe ni mchezo na
kadhalika. Chochote kile kinachokufanya ujisikie vizuri ni kitu muhimu sana
kwako.

Baada ya kujua kitu hiki panga ni vipi unaanza kukifanya. Jua
kwa sasa upo wapi na utaanzia wapi ili kufika wapi.

Kisha tenga muda kila siku wa kufanya kitu hiki. Kama
kinahusiana na biashara, tenga muda kila siku wa kufanya biashara hiyo. Huna
haja ya kuanzia mbali, anza kidogo na anza kwa kutafuta mteja mmoja, mpatie
bidhaa au huduma nzuri na hakikisha unabadili maisha yake kupitia kile
unachofanya. Tafuta tena mteja mwingine na fanya kama ulivyofanya kwa mteja wa
kwanza na endelea kuboresha. Wakati huu bado unaendelea na kazi yako hivyo
hujali sana kuhusu kipato, bali kutoa kitu bora ambacho kitawafanya wengine
wakuzungumzie.

Ukiendelea hivi kwa muda, miaka kadhaa utafikia kuwa na wateja
wengi kiasi kwamba kipato unachopata kwenye ajira yako ni kidogo ukilinganisha
na hiki cha pembeni. Na hapo unakosa muda wa kuwahudumia wateja wako wote. Hapa
ndio unaacha kazi na kufanyia kazi kitu hiko moja kwa moja.

Uko makini na umejitoa kutengeneza kitu kama hiki na unahitaji
muongozo zaidi? Tuwasiliane, niandikie email kwenye makirita@kisimachamaarifa.co.tz na niambie ni
nini unataka kufanya na tutajadili jinsi ya kuweza kupata muongozo mzuri. Ukiwa
mwenyewe ni rahisi kukata tamaa, ukiwa na mwongozo utapata hamasa ya kwenda
zaidi.

TAMKO LA LEO;

Najua ninachofanya sasa sio kile ambacho napenda kufanya bali
ambacho kila mtu anategemea nifanye, ili nipate kipato cha kuendesha maisha.
Sasa nimeamua kutenga muda kila siku na kuanza kufanyia kazi kile ambacho
ninapenda kufanya. Nitaweka juhudi kubwa kwenye kitu hiki na najua kwa muda wa
mbeleni kitakuwa chanzo changu kikubwa cha mapato.

Tukutane kwenye ukurasa wa 175 kesho, Like page yangu ya
Coach
Makirita Amani
uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha
kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365
bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo
maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya
facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya
email.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na
KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata
utaratibu.

TUPO PAMOJA.