Kama unaendesha biashara ndogo, au unaendesha biashara mpya ambayo tayari kuna watu wengine ambao wanaifanya biashara hii kwa muda mrefu na wana mtaji mkubwa kuliko wewe, basi una njia nyembembe sana ya kuweza kufanikiwa.

Ukweli ni kwamba hawa waliopo kwenye biashara hiyo kwa muda mrefu na wana mtaji mkubwa kuliko wewe wana nafasi kubwa sana kiushindani kuliko wewe. Wanaweza kutumia fedha nyingi kwenye matangazo wewe huwezi. Wanaweza kutoa zawadi nyingi kwa wateja wewe huwezi.

Kwa vyovyote vile kuingia kwenye biashara ambayo kuna watu wachache wameitawala inaweza kuonekana ni kama kujiingiza kwenye shimo la simba. Lakini leo nataka nikupe siri moja ambayo itakuwezesha kufanikiwa kwenye biashara hata kama mshindani wako ni mkubwa kiasi gani.

Kwanza kabisa ni lazima ukubali kwamba huwezi kumzidi mshindani wako huyo kwa matumizi ya fedha, huwezi na sahau kuhusu hilo. Ila unaweza kumzidi kwa vitu muhimu sana. Unaweza kumzidi kwa kazi, unaweza kumzidi kwa ubunifu na unaweza kumzidi kwa huduma bora sana kwa wateja wako.

SOMA; Jinsi Ya Kujua Kama Unachofanya Ni Sahihi Katika Maisha Yako.

Fanya kazi mara mbili ya wanavyofanya watu wengine waliopo kwenye biashara hiyo. Ndio nimesema mara mbili. Kama wenzako waanza kazi saa mbili na kufunga saa kumi, wewe anza saa kumi na mbili na funga saa mbili usiku. Hakikisha unakuwa mbele sana kwenye kazi unayofanya kwenye biashara yako.

Kuwa mbunifu sana, tatizo la biashara kubwa ni kwamba hawapo tayari kubadili vitu haraka. Ila wewe mwenye biashara ndogo unaweza kubadili kitu chochote kwa haraka sana. Tumia nafasi hii kujaribu kila aina ya ubunifu ili kutoa kilicho bora kwa wateja wako.

Toa huduma bora sana kwa wateja wako. Kadiri biashara inavyokua ndivyo huduma kwa wateja inazidi kuwa mbovu. Sasa wewe wa biashara ndogo hakikisha unamjua mteja wako kama rafiki yako. Tengeneza urafiki mzuri kati yako na wateja wako na itakusaidia sana kufanikiwa.

Kumbuka unafanya haya yote sio kwa ajili ya kushindana na biashara kubwa, ila kwa ajili ya kuwa bora sana kuliko mtu mwingine yeyote anayefanya biashara hiyo.

Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.

Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.

Jiunge na COACHING/MENTORSHIP PROGRAM ambapo utapata muongozo wa hatua kwa hatua mpaka ufikie mafanikio kwenye kazi au biashara unayofanya. Bonyeza haya maandishi kupata maelekezo ya programu hii.