Kama jibu lako ni sina mteja basi jitathmini vizuri.
Kwanza kabisa kila mmoja wetu ana mteja, kama wewe ni mtu mzima na unaishi basi una mteja au una wateja wengi sana. Wateja hawaishii kwa wafanyabiashara tu. Wateja wapo kwa kila mtu.
Kama wewe ni mfanyabiashara, mteja wako au wateja wako wazi, ni wale wanaonunua kutoka kwako.
Kama wewe ni mwajiriwa mteja wako ni bosi wako au yeyote aliye chini yako.
Kama wewe ni meneja basi una wateja wawili wakuu. Kwanza wale walioko juu yako, wakurugenzi na kadhalika na wale walioko chini yako, yaani wafanyakazi unaowasimamia.
Kama wewe ni kiongozi basi wateja wako ni wafuasi wako.
Na kama wewe ni kiongozi wa dini basi waumini ni wateja wako.
SOMA; KILA MTU ANAUZA, JE WEWE UNAUZA NINI?
Sasa turudi kwenye swali la msingi, je umemridhisha mteja wako leo? hili ni swali muhimu sana la wewe kujiuliza kila siku. Na jibu utakalojipa litakuwezesha kuboresha zaidi kile ambacho unatoa kwa mteja wako.
Kitakachokuwezesha kufanikiwa kwenye kazi, biashara na hata maisha ni ubora wa huduma unazotoa kwa wale wanaozitumia. Ndio maana kumridhisha mteja ni jukumu lako namba moja.
Jiulize leo ni mambo gani umefanya ambayo yamemridhisha mteja na kufanya maisha yake kuwa bora. Pia jiulize ni mambo gani umefanya ambayo sio mazuri kwa mteja ili usiyarudie tena kesho.
Mimi leo nimemkumbusha mteja wangu(wewe) kumjali mteja wake, wewe je?
Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.
Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.
Jiunge na COACHING/MENTORSHIP PROGRAM ambapo utapata muongozo wa hatua kwa hatua mpaka ufikie mafanikio kwenye kazi au biashara unayofanya. Bonyeza haya maandishi kupata maelekezo ya programu hii.