Tulishasema kwamba jambo muhimu kabisa kwenye biashara ni kujua mteja wako ni nani. Kama upo kwenye biashara na humjui mteja wako basi hujui ni nini unafanya kwenye biashara yako. Na ninaposema kumjua simaanishi kumjua kwa jina, bali kujua sifa za mteja wako kuanzia umri, kipato, anakoishi na mengine kama hayo. Hivyo kama bado hujamjua mteja wako ishia hapa kwa sasa na fungua kusoma makala hii; Vitu Viwili Muhimu Kujua Kuhusu Wateja Wa Biashara Yako, baadae utarudi kuendelea kusoma hapa.

Kama tayari umeshamjua mteja wako sasa swali linakuja muhimu, je biashara yako inaendana na mteja wako. Je mteja anaona hii ni aina yake, hiki ndicho anachojali? Je ni kitu ambacho anaweza kukiongelea kwa ufahari mbele ya wenzake na wakaona kweli ni kitu muhimu anafanya au amenunua?

Unahitaji kuwa na biashara ambayo inamfanya mteja kujiona ni sehemu muhimu ya biashara hiyo. Unahitaji kumfanya mteja wako kuwa mtu wa kwanza kutangaza biashara yako. Fanya hivi kwa kuhakikisha kila unachofanya kwenye biashara yako kinaendana na mteja wako.

Nakutakia kila la kheri kwenye biashara yako.

Kipengele hiki cha BIASHARA LEO kinakupa mbinu muhimu za kutatua changamoto za kibiashara zinazokuzuia kufikia mafanikio makubwa. Pia unajifunza kuepuka makosa unayofanya kwenye biashara yako na yanakuzuia kufanikiwa. Kujifunza mengi zaidi kuhusu mafanikio kwenye maisha jiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa kubonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Kwa ushauri zaidi wa kibiashara, ikiwepo jinsi ya kupata wazo bora la biashara, jinsi ya kuanza na kukuza biashara na jinsi ya kupambana na changamoto za biashara piga simu 0717396253.

Jiunge na COACHING/MENTORSHIP PROGRAM ambapo utapata muongozo wa hatua kwa hatua mpaka ufikie mafanikio kwenye kazi au biashara unayofanya. Bonyeza haya maandishi kupata maelekezo ya programu hii.