image

Mara nyingi watu wamekuwa wakijikuta kwenye wakati mgumu sana.
Hii ni baada ya kuingia kwenye fursa ambayo waliambiwa ni nzuri ila wanapoingia wanakutana na changamoto nyingi sana.
Fursa nzuri sana ni ile ambayo unaitengeneza mwenyewe, au unaitafuta mwenyewe na unaweza kuifanya kwa utofauti.
Kama fursa umeisikia kwa wengi mara nyingi unakuwa umeshachelewa.
Ila pia una nafasi ya kuitumia fursa vizuri kama utaongeza utofauti, utaweka ubunifu wako na kama utakwenda hatua ya ziada.
Ila kama umesikia fursa inalipa, na wewe ukakimbilia kuifanya, tena kwa mtindo ule ule ambao kila mtu anaifanya, pole sana maana umenunua tiketi ya kwenda kushindwa.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani