Wakati wewe unakazana kuboresha maisha yako na kufikia mafanikio, kuna watu watakuchukia bila sababu yoyote ile.
Wakati wao wanapoteza muda na wewe ukaacha kupoteza nao muda, watakuchukia.
Wakati wao wanafanya matumizi makubwa kuliko vipato vyao na wewe ukakwepa hilo, watakuchukia.
Wakati wao wanafanya kazi kwa kawaida tu na hawamalizi mpaka dakika za mwisho, huku wewe ukifanya kwa ubora wa hali ya juu na kumaliza haraka, watakuchukia.
Hujagusa maisha yao lakini wao wanakuchukia.
Unajua ni kwa sababu gani?
Kwa kuwa wanaoshindwa wanapenda kuona wanaowazunguka nao wanashindwa.
Hivyo usiumizwe na chuki zao, ila hakikisha unakuwa mbali nao ili wasije kukuambukiza tabia zao hizo.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani.
Kama Unayapigania Mafanikio, Watu Watakuchukia, Usiumizwe na Hilo.
