Kama lengo lako litakuwa kukimbiza fursa mpya kila wakati, basi maisha yako yatakuwa ya mbio tu.
Fursa mpya zipo na zinaendelea kuibuka kila wakati. Huwezi kuwa unarukia kila kitu kipya kinachokuja, utafanya hivyo mpaka lini?

Ni kweli kunaweza kuwa kunakuja fursa nzuri sana. Kunaweza kuwa kunakuja fursa za kipekee ambazo hujawahi kuziona. Lakini kama maisha yako yote yatakuwa ya kuangalia ni ipi fursa mpya uiendee, yatakuwa magumu sana.
Ni lazima ufike mahali uamue kwamba utafanya vitu fulani tu. Kwa kuamua huko unachagua kuwa bora sana kwenye vitu hivyo. Na kuanzia hapo utaziangalia fursa mpya zinazoendana na eneo hilo ulilochagua.
Chagua eneo ambalo utajiendeleza vizuri na kuwa bora, na uache kukimbiza kila fursa. Kuna wakati hutakuwa na nguvu tena za kukimbiza kila fursa, maisha yako yatakwendaje?
TAMKO LA LEO;
Najua ya kwamba dunia ina fursa nyingi na nzuri sana zinazoibuka kila siku. Najua ya kwamba fursa hizi zinanivutia sana kuwa ninazikimbiza. Ila najua ya kwamba siwezi kuwa nakimbiza fursa mpya kila wakati. Nahitaji kuchagua eneo ambalo nitalifanyia kazi vizuri. Niache kukimbiza kila fursa bali niziendee fursa zilizopo kwenye lile eneo nililochagua. Muda wangu haunitoshi kukimbiza kila fursa, nitautumia vizuri kwenye fursa chache nitakazochagua.
Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Pia usiache kutembelea mtandao huu kila siku kujifunza mambo mapya na mazuri. Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.