Sisi binadamu ni viumbe wa kijamii. Kwa miaka mingi tumekuwa salama kwa kuwa ndani ya jamii, kwakufanya kile ambacho kila mtu anafanya.
Lakini miaka ya sasa hakuna hatari kubwa hata kama hutaenda na kundi, lakini bado watu wengi wanajisikia salama zaidi wanapofanya kitu ambacho kila mtu anafanya.

Kufanya kitu ambacho kila mtu anakifanya, ni kweli kuna usalama kwa kuwa na hakika kwamba ndio kitu kinachotegemewa. Kama ni kazi basi ndio inavyofanyika na utalipwa, kama ni biashara basi ndivyo inavyofanyika na utapata wateja.
Lakini kuna mtego mmoja kwenye hili, ni rahisi na salama kufanya kile ambacho kila mtu anafanya, ila ni vigumu sana kufikia mafanikio makubwa kwenye kitu hiko.
Huwezi kupata mafanikio makubwa kwa kufanya kile ambacho kila mtu anafanya na kwa kukifanya kwa mtindo ule ule ambao kila mtu anafanya. Ni kazi kubwa sana kwa sababu kila mtu anafanya hivyo na hakuna cha tofauti kinachokutenga au kukutofautisha.
SOMA; Matatizo Yote Ya Mahusiano Huanzia Hapa.
Ufanye nini sasa?
Uache kufanya kile ambacho kila mtu anafanya? Hapana, huenda ndio unachopenda kufanya.
Badala ya kuacha kabisa, amua kufanya kwa utofauti, amua hata kufanya kinyume na kila mtu anavyofanya, amua kujiweka tofauti kiasi kwamba unakuwa wa tofauti na wa pekee.
Na utofauti tunaozungumzia hapa sio tu kuwa na vitu tofauti, bali kutoa thamani tofauti, ambayo mtu hawezi kuipata sehemu nyingine yoyote.
Na hapa utajiweka pembeni na kundi, utapunguza ushindani usio na maana na utakuwa kwenye safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa.
Lakini sio rahisi kufanya hivi, inahitaji ujasiri, inahitaji kujitoa, inahitaji nidhamu na ndio maana ni wachache walioweza kufanya vitu vya tofauti na kuwa na mafanikio makubwa.
Na wewe ni mmoja wa watu hao, nakuamini, nenda ukawe tofauti.
TAMKO LA LEO;
Najua kile ninachofanya karibu kila mtu anaweza kukifanya, na wengi wanafanya. Najua mafanikio makubwa hayatakuja kwangu kwa kufanya kile ambacho kila mtu anafanya na kwa mtindo ule ule. Hivyo nimeamua kufanya kwa tofauti kwa kuongeza thamani kubwa sana ili watu wapate kitu bora ambacho hawawezi kupata sehemu nyingine yoyote. Chochote nitakachogusa, nahakikisha kinakuwa bora sana.
Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Pia usiache kutembelea mtandao huu kila siku kujifunza mambo mapya na mazuri. Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.