Moja ya hatua muhimu sana unazotakiwa kupiga ili kuweza kufikia mafanikio makubwa ni kuacha kulalamika au kulaumu wengine. Haijalishi ni nani au nini kimefanya nini, haijalishi ndugu zako wamekufanyia nini, haijalishi serikali imefanya nini, utakapoanza tu kulaumu na kulalamika, umejiondoa kwenye njia ya mafanikio.
Hivyo kila linalotokea unapaswa kulibeba na wewe mwenyewe kuchukua hatua ya kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi.

Sasa kuna kitu kingine kibaya sana watu wamekuwa wanafanya na kinawazuia kufikia mafanikio. Kitu hiki ni kujilaumu sana wao wenyewe, kujisema na kujishusha mpaka kufikia hatua ya kujiona hufai.
Kama utakuwa mtu wa kujilaumu kila mara, kwa kujiona huwezi, kwa kujiona hufai, kwa kitu kutokea na kusema nilijua tu sitaweza, kwa kujiona una kisirani, ni vigumu sana kufikia mafanikio makubwa.
SOMA; Angalia Nyuma Kwa Lengo Moja Tu…
Kila mmoja wetu anapitia changamoto mbalimbali kwenye maisha, usikubali changamoto unazopitia zikugeuze wewe kujiona ni mtu wa hovyo sana. Hata kama umefanya kosa kubwa, jifunze kupitia kosa lile na songa mbele. Kukaa kujilaumu kwa makosa ambayo umeshafanya hakutakusaidia kwa namna yoyote zaidi ya kukuondolea kujiamini na kukuzuia kufikia mafanikio.
TAMKO LA LEO;
Najua nimekuwa adui wa mafanikio yangu mwenyewe kwa kujilaumu kupita kiasi. Nimekuwa najiona siwezi na sifai, nimekuwa nakaribisha kushindwa kila mara kwa kufikiri mawazo ya kushindwa tu. Kuanzia sasa sitapoteza tena muda wangu kujilaumu au kujiona sifai. Kosa lolote nitakalofanya nitajifunza kupitia kosa hilo na nitasonga mbele. Kujilaumu hakuna tena nafasi kwangu.
Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Pia usiache kutembelea mtandao huu kila siku kujifunza mambo mapya na mazuri. Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.