Maana yake unajua kabisa ya kwamba kuna vitu vingine vingi unataka, lakini hiki ni muhimu zaidi.

Unajua ya kwamba kuna vingi vitakuja njiani lakini hutaacha hiki ulichoamua kwa sababu ya vitu hivyo.

Unajua ya kwamba utakutana na changamoto nyingi lakini hutakubali zikurudishe nyuma.

Unajua kabisa ya kwamba kuna wengi watakukatisha tamaa na kutaka kukurudisha nyuma lakini wewe hutakubali.

Hivi ndivyo maamuzi yalivyo magumu, na ndio maana ni wachache sana wanaoweza kufanya na kusimamia maamuzi yao. Na hawa ndio washindi.

Je na wewe ni mmoja wa watu hawa?

Fanya maamuzi, yasimamie, jitoe na usikubali kurudi nyuma.

SOMA; Usifanye Maamuzi Yako Kwa Kigezo Hiki, Utajuta Sana…

TAMKO LANGU;

Najua kufanya maamuzi na kuyasimamia sio kazi ndogo. Na ndio maana wachache sana ndio wanaoiweza. Mimi ni mmoja kati ya watu hawa wachache. Nitafanya maamuzi sahihi kwangu na kuyasimamia, lije jua ije mvua, iwe usiku au iwe mchana, mwisho wangu ni pale nitakapofikia ninachotaka na sio tofauti na hapo. Haya ndiyo maamuzi nitakayoishi nayo.

NENO LA LEO.

A wise man makes his own decisions, an ignorant man follows the public opinion.

Grantland Rice

Mtu mwerevu hufanya maamuzi yake mwenyewe, mtu mjinga hufuata maoni ya watu wengine.

Rafiki na Kocha Wako,

Makirita Amani,

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

TUPO PAMOJA.