Habari za leo rafiki?

Naamini uko poa sana, rafiki yako niko vizuri sana.

Karibu tena kwenye mazungumzo yetu haya muhimu sana kama marafiki. Karibu tushirikishane yale muhimu katika safari yetu hii tuliyochagua, safari ya kuwa tofauti na kuwa bora sana kila siku.

Leo nataka tushirikishane jambo moja muhimu ambalo limekuwa linapoteza watu wengi sana. Kuna watu wengi ambao wamekuwa akijibania nafasi ya kusonga mbele zaidi ya pale walipo sasa kwa sababu ambazo hata sio za msingi.

Huwa nawaambia watu kwamba kujifunza kila siku ni hitaji muhimu na la msingi katika kuboresha kile unachofanya na maisha kwa ujumla. Lakini kuna watu ambao huwa wanasema, hakuna kitu kipya cha kujifunza, yote ni yale yale ambayo tayari tunayajua.

Na mimi nakubaliana nao ni kweli kabisa hakuna jipya, karibu yote ni yale yale ambayo yamekuwepo tangu enzi na enzi. Lakini bado unahitaji kujifunza kila siku, naweka msisitizo; KILA SIKU.

Ndio mambo hayo hayo ambayo unafikiri unayajua, unahitaji kuendelea kuyasoma na kujifunza kila siku.

HAKUNA JIPYA.

Jana nilikuwa nasoma kitabu ambacho kimejadili misingi mikuu ya dini nne kubwa duniani. Kwenye kitabu hiki waliangalia ni kitu gani ambacho dini hizi zinacho kwa pamoja. Dini zilizojadiliwa kwenye kitabu hiko ni Ukristo ambapo kiongozi mkuu alikuwa Yesu, dini ya Ubudha ambapo kiongozi mkuu alikuwa Budha, dini ya Uhindu, ambapo kiongozi mkuu alikuwa Krishna na dini ya Tao ambapo kiongozi mkuu alikuwa Lao Tzu.

Nilichojifunza ni kwamba dini zote hizi zinazungumzia ujumbe mmoja mkuu, na ambao watu wengi kwa sasa hawafanyi, licha ya dini hizi kuwepo kwa muda mrefu. Kingine nilichojifunza ni kwamba Budha alikuwepo kabla ya Yesu, na wote waliishi vipindi tofauti na katika nyakati tofauti, lakini wote mafundisho yao yalikuwa yanafanana sana. Wote walizungumza vitu ambavyo vinaendana.

Hatutaenda ndani sana kujadili mengi niliyojifunza, lakini nataka upate picha kwamba haya tunayofanya kwa sasa sio mapya, yalikuwepo miaka mingi sana kabla hata ya kuja kwa Yesu. Na kama umekuwa muumini tangu utoto mpaka sasa utakuwa unajua kabisa ya kwamba amri ni zile zile, hazijabadilishwa, lakini bado unatakiwa kukumbushwa kila mara.

Kwa mfano kwa Wakristo, amri ni kumi tu, lakini imekuwa ni shida sana kuweza kuzifuata. Na kama kila mtu angeweza kufuata amri hizi kumi, maisha yangekuwa bora sana kwa kila mtu hapa duniani. Lakini wengi sana hawawezi kuzifuata na ndipo matatizo yanapoanzia.

UNAHITAJI KUAMBIWA TENA NA TENA NA TENA…

Ndio hakuna jipya, ndio unayajua yote haya, lakini unahitaji kuambiwa tena na tena na tena.

Labda tuanze na kitu cha kawaida ambapo tutaelewana vizuri zaidi.

Najua lazima utakuwa unatumia mtandao mmoja au zaidi wa simu kati ya TIGO, AIRTEL au VODACOM. Na huenda umekuwa unatumia mtandao huo kwa zaidi ya miaka kumi sasa (namba yangu ya tigo naitumia kwa zaidi ya miaka 10 sasa). Sasa nikuulize swali muhimu, imewahi kupita siku hujasikia tangazo la Tigo au Voda au Airtel?

Fungulia redio yako na kila baada ya muda mfupi utasikia tangazo, pita barabarani na utaona mabango, angalia tv utaona matangazo, na hata pale makampuni haya yanapodhamini mashindano au kutoa misaada, utaona kila sehemu kuna nembo ya kampuni hiyo. Wakati mwingine kampuni inaweza kuomba watu wenye uzio wa ukuta kupata ukuta huo rangi na kuweka matangazo yao.

Unajua kwa nini wanafanya haya yote? Japo wana wateja wengi ambao wataendelea kuwa nao, lakini kwa nini waendelee kuwapigia kelele?

Hapa wanatumia mbinu muhimu sana ya kisaikolojia, kuhakikisha wewe kila unapofikiri mawasiliano unafikiri kampuni fulani tu, kwa sababu ndio imekuzunguka, ukifungua redio unasikia, ukiangalia tv unaona, ukitembea unaona mabango. Kisaikolojia unabaki kuifikiria kampuni hiyo zaidi.

Sasa hii ndio mbinu ambayo hata wewe unahitaji kuitumia ili uweze kufikia chochote unachotaka.

Licha ya kujua, licha ya kuona haya sio mapya, unahitaji kujifunza kila siku, kila unapofikiri unakuwa unafikiri kwa misingi hiyo uliyojifunza. Kwa njia hii utaona mambo yako yanakwenda vizuri. Unapokutana na changamoto huanzi kulalamika na kukata tamaa, badala yake unakumbuka ulivyojifunza changamoto za aina fulani zinafanyiwa hivi na hivi, unaanza kuchukua hatua na unasonga mbele.

Ndio maana nasisitiza sana, tena sana, usikubali siku ipite bila ya wewe kujifunza kitu chochote cha kufanya maisha yako kuwa bora sana.

NI SEHEMU GANI YA UHAKIKA KWANGU KUJIFUNZA KILA SIKU?

Karibu kwenye KISIMA CHA MAARIFA na uwe mwanachama wa GOLD, hapo unakuwa umekata tiketi ya safari ya uhakika ya kujifunza kila siku, ndio yaani kila siku utakuwa na vitu vingi vya kujifunza. Na kujifunza kweli kunaanza na wewe mwenyewe kutafakari maisha yako, ulikotoka, ulipo, unapokwenda, unachofanya na unachotarajia kupata.

Karibu sasa kwenye KISIMA CHA MAARIFA na kila siku utapata mbinu bora za kukuwezesha kutumia kile unachojua kufika mbali zaidi.

Najua umeshajifunza mengi sana, lakini kwa nini huyafanyii kazi?

Unajua kabisa ya kwamba unahitaji kuwa unajilipa wewe mwenyewe, kwa kuweka pembeni asilimia 10 ya kipato chako, lakini mbona hufanyi?

Unajua kabisa ya kwamba muda ndio kitu adimu na cha thamani sana, na unahitaji kutumia muda wako vizuri, lakini mbona bado unaendelea kupoteza muda?

Haya mambo sio rahisi na ndio maana unahitaji kuwa kwenye mazingira ambayo yanaendelea kukusisitiza kwenye hilo.

Na hatari nyingine kubwa ni kwamba umezungukwa na watu ambao wanakuvuta chini, watu ambao ukiwaambia ndoto yako kubwa watakucheka sana na kukuambia acha ujinga, watu ambao wakiona unawaacha wanaanza kukusema maneno mabaya. Watu ambao wanataka ufanye kile ambacho wao wanafanya hata kama hakina manufaa kwao.

Unahitaji nguvu ya ziada kuweza kuvuka yote haya, na nguvu hiyo utaipata kwa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA, hasa kwenye kundi la wasap ambalo unapata nafasi ya kushirikiana na wengine ambao wapo kwenye safari kama yako.

JIUNGE NA KISIMA CHA MAARIFA.

1. BONYEZA HAYA MAANDISHI NA JAZA FOMU, weka taarifa zako vizuri.

2. Tuma ada ya uanachama tsh elfu 50 kwa mwaka, tangu tarehe uliyojiunga. Ada tuma kwenye namba 0717396253 au 0755953887.

3. Tuma ujumbe kwenye moja ya namba hizo wenye majina na email uliyojiunga nayo. Na kama unatumia wasap tuma ujumbe kwa wasap kwenye namba 0717396253

4. Karibu kwenye KISIMA CHA MAARIFA na ujifunze na kufanyia kazi yale ambayo ni muhimu sana.

Fanya hivyo leo, au hutafanya kabisa na kujikosesha nafasi hii nzuri ya kuyafanya maisha yako kwenda mbele zaidi.

Nakutakia kila la kheri kwenye safari hii uliyochagua, ni safari ya kipekee sana, usishangae pale wengine watakapokuwa hawakuelewi.

Rafiki na kocha wako,

Makirita Amani,

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

AMKA CONSULTANTS