Habari za leo rafiki?
Naamini upo vizuri sana na maisha yako yanaendelea kuwa bora kadiri siku zinavyokwenda. Vizuri na hongera sana kwa hilo.
Karibu tena kwenye mazungumzo yetu haya mazuri na muhimu sana, ambapo tunashirikishana mambo mbalimbali yanayohusu mafanikio na kuwa na maisha bora.
Leo nitakushirikisha swali moja muhimu sana ninalojiuliza kila siku asubuhi na hata siku nzima ambalo kwa kiasi kikubwa limeniwezesha kufanya mambo makubwa. Ni swali rahisi sana ambalo hata wewe mwenyewe unaweza kuwa unajiuliza kila siku na ukaona manufaa yake mazuri kwenye maisha yako.
Ukianza kujiuliza swali hili utaona siku zako zinaanza kuwa bora, utaona mtazamo wako wa maisha unakuwa tofauti kabisa na ulivyokuwa nao hapo mwanzo. Na mambo yote uliyokuwa unaona magumu yanaanza kuwa marahisi.
Na vizuri zaidi ni kwamba mimi kama rafiki yako, nitakupa njia nzuri sana ya kuhakikisha husahau kujiuliza swali hili kila siku, yaani nitakuwa pembeni yako kila siku kuhakikisha umejiuliza swali hili.
Je upo tayari kulijua swali hili na kuchukua hatua kuhakikisha kwamba hukosi nafasi ya kuweza kujiuliza swali hili kila siku? Karibu sana. Ila kwa dakika chache sana naomba nikushirikishe ujumbe huu mzuri niliotumiwa na rafiki yetu ambaye ni msomaji mwenzetu;
Habari rafiki yangu,
Naamini unaendelea vizuri lakini pia inawezekana hauko vizuri kiafya pia ila kutokana mafunzo ambayo umekuwa ukinipa kupitia mitandao iliyo chini yako naamini huwezi kukata tamaa, lengo la ujumbe huu ni kukujulisha ni jinsi gani nilivyopata hamasa kubwa kuliko siku zote kupitia makala uliyoitoa leo tarehe 20/11/2015 iliyokuwa ikihusu yale uliyojifunza kupitia kiongozi wa kisiasa na aliyekuwa mgombea uraisi kwa tiketi ya chadema, kwa mtizamo wangu nimeuona uwezo mkubwa sana ulionao na pengine nafikiri umebeba maajabu mazuri na makubwa sana kichwani mwako, naomba nikupe pongezi kwa hili kwa sababu naona kabisa unakwenda kuifikia nafasi ambayo haijawahi kufikika na mtu mweusi duniani hapa, siandiki haya kwa kukuvisha kilemba cha ukoka ila naandika haya kuthibitisha yale ninayoyaona, ninayojifunza na kuyafanyia kazi na hatimaye kunipa majibu ambayo ni kupitia maandiko yaliyotoka kichwani mwako nakwenda kutoa nakala ya makala hiyo ya leo na nakuthibitishia kuwa nitajifunza kwa vitendo usiku na mchana mpaka nitakapofikia viwango bora na vikubwa (kimataifa) kupitia hii.
Mwisho naomba nikujuze tu kwamba tuko pamoja katika safari hii ambayo tayari imeanza kwa kasi, vilevile napenda kukuthibitishia kuwa kule unakotaka kufika utafika tu tena kwa kishindo kikubwa.
Zanuni N.
Kwanza nichukue nafasi hii kumshukuru sana rafiki yetu na hata wewe rafiki yangu kwa kuendelea kuwa pamoja hapa. Naamini kuna kitu kikubwa unachopata na ndio maana mpaka sasa tupo pamoja. Nimpongeze sana rafiki yetu kwa maamuzi mazuri aliyofanya kwamba amejitoa kufanya kwa vitendo usiku na mchana kuhakikisha anafikia viwango vikubwa sana vya ubora. Hii ni kauli nzito sana ambayo haiwezi kuzuiwa na chochote. Na yeyote anayeitoa kauli hii na kuifanyia kazi, hakuna kinachoweza kumzuia kuwa bora sana.
Nawaahidi marafiki zangu wote kwamba tupo pamoja na tutaendelea kuwa pamoja, safari hii tumeshaichagua na hakuna kitakachoturudisha nyuma, nakili haya maneno yangu na yatumie kwako pia.
Swali muhimu ninalojiuliza kila siku.
Sasa karibu nikushirikishe swali ambalo huwa najiuliza kila siku asubuhi na hata siku nzima. Kwa swali hili moja nimekuwa naweza kupata mada mbalimbali za kuandika ambazo zinanisaidia mimi binafsi na ninyi marafiki pia.
Kama unavyojua wewe rafiki yangu, na najua unajua kwa sababu umekuwa unasoma hapa kila mara, huwa naandika kila siku. Na huwa nikiona mtu anaandika huwa namshauri sana aandike kila siku, yaani kila siku, haijalishi ni jamatano au jumapili, haijalishi ni krismasi au idd, muhimu ni kuandika kila siku. Sasa wengi ninaowashauri hivi huwa wananiuliza nitapata wapi vitu vya kuandika kila siku? Na jibu langu huwa ni hili moja, FUNGA MDOGO, KAA CHINI NA ANDIKA.
Na huwa nawashirikisha swali hili muhimu sana ninalojiuliza kila siku, swali hili ni; NI UJUMBE GANI MUHIMU NA MZURI NINAOWEZA KUWASHIRIKISHA WATU LEO? na ujumbe huu ni ule ambao unamfanya mtu aweze kuchukua hatua ya kuboresha maisha yake zaidi.
Haijalishi kama ujumbe ni mkubwa au mdogo, haijalishi kama ujumbe ni mpya au unaojulikana tayari, kikubwa ni kutoa ujumbe mzuri ambao utamfanya mtu aweze kuchukua hatua hata kama ni ndogo sana.
Kwa kujiuliza swali hili unaanza kuangalia kila eneo la maisha yako ambapo unaweza kupata ujumbe mzuri, labda ni kitabu ulichosoma karibuni, labda ni tukio uliloshuhudia, labda ni uzoefu ulionao, labda ni hali fulani inayoendelea. Kwa kuangalia kila eneo la maisha yako, huwezi kukosa ujumbe mzuri wa kuwashirikisha wengine kila siku.
Unatumiaje swali hili kwenye maisha yako na kazi zako?
Unaweza kujiuliza swali hili kwa kazi au biashara yoyote unayofanya.
Unachofanya ni kila siku unapoamka asubuhi, jiulize ni kitu gani kizuri na kinachoweza kuwasaidia watu unaweza kufanya leo kwenye kazi yako au biashara yako? hata kama ni kitu kidogo sana, lakini unapofanya vitu hivi vidogo kila siku, siku moja vinakuja kuonekana vikubwa sana.
Je upo tayari kujiuliza swali hili kila siku?
Upo tayari kufikia mafanikio makubwa sana, na kwa kuanza kwa kujiuliza swali hilo kila siku? Kama upo tayari basi hongera sana.
Lakini kabla hujajiaminisha hivyo nikuambie kitu kimoja muhimu nilichojifunza kwa uzoefu, wengi husema wapo tayari na huanza siku chache za mwanzo, lakini baadae wanasahau na kurudi kwenye maisha yao ya kawaida. Na hivyo kushindwa kufaidi nguvu hii nzuri sana ya kubadili maisha yao.
Njia ya kukuhakikishia unajiuliza swali hili kila siku.
Kuna njia ya uhakika sana ambayo itakuhakikishia wewe kuweza kujiuliza swali hili kila siku. Si unakumbuka mimi huwa najiuliza hivi kila siku? Basi wakati mimi najiuliza na wewe pia utajiuliza, yaani tutajiuliza kwa pamoja. Huoni itakuwa vizuri sana? Kama jibu ni ndio basi karibu tuwe tunajiuliza pamoja.
Unapataje nafasi hii ya kujiuliza pamoja?
Kwa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, na kulipia ada ya uanachama wa GOLD, unapata nafasi ya kuingia kwenye kundi la wasap ambapo huko kila siku asubuhi utakumbushwa kujiuliza swali hili muhimu la siku yako na pia unapata tafakari nzuri ya maisha yako kila siku. Kuna mengine mengi na mazuri ya kujifunza kupitia kundi hilo.
Unawezaje kujiunga na kundi hilo la wasap?
Kwanza uwe unatumia wasap.
Pili lipa ada ya uanachama wa GOLD ambayo ni tsh elfu 50(50,000/=) kwa mwaka kwenye namba 0717396253 au 0755953887.
Tatu tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253 wenye majina yako.
Nne utawekwa kwenye kundi na kupewa maelekezo mengine ya kukamilisha kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.
Kama unataka nafasi hii ya kufanya maisha yako kuwa bora kila siku basi jiunge leo hii, ukisema unasubiri, utasahau, halafu utarudi kule ambapo umetoka.
Kuna makala mbili nataka uzisome, kama bado hujazisoma. Makala hizi ni muhimu sana kwani zinakupa maarifa muhimu ya wewe kuweza kuchukua hatua ya kuboresha maisha yako.
Makala ya kwanza ni hiyo ambayo msomaji mwenzetu ameandika maoni yake tuliyosoma hapo juu, na hii nimekushirikisha mambo 10 niliyojifunza kutoka kwa Edward Lowassa, tafadhali sana isome hapa; Mambo Kumi (10) Kuhusu Maisha Na Mafanikio Niliyojifunza Kutoka Kwa Edward Ngoyai Lowassa.
Makala ya pili ni ushauri kuhusu kipi cha kufanya kwanza, kati ya kuoa, kuendelea na masomo au kujenga, kuna mengi ya kujifunza pia hapa. Soma; USHAURI; Kuendelea Na Masomo, Kuoa Au Kujenga, Kipi Bora Kufanya Kwanza?
Fanyia kazi haya ambayo unajifunza rafiki yangu. Na kama bado hujaingia kwenye kundi la KISIMA CHA MAARIFA, usitake na leo pia ipotee bila ya kuchukua hatua, fanya hivyo sasa.
Nakutakia kila la kheri rafiki yangu, tupo pamoja na tutaendelea kuwa pamoja.
Rafiki na kocha wako,
Makirita Amani,