Tunaishi kwenye dunia ya mwendo kasi, kila kitu kinakwenda kwa kasi kubwa sana. Kwa mwendokasi huu tumeshapata dhana kwamba ukisubiri kidogo tu, unaachwa nyuma. Hivyo tumejikuta wote tunakimbia kimbia wakati mwingine hatuna hata uhakika tunakimbiza nini.

Tunakimbia tu ili na sisi tuonekane tupo kwenye mbio. Katika kukimbia huku tumekuwa tunakosa hata muda wa kukaa na kuyatafakari maisha yetu, kutafakari maisha kwa ujumla na kutafakari kile ambacho tunakifanya. Kwa kukosa nafasi hii ya kutafakari, tumekuwa tunafanya mambo kwa mazoea yale yale na kushindwa kuzijua na kuzitumia fursa mpya zinazojitokeza.

Makala hizi za kurasa, pamoja na KITABU CHA KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO, ni sehemu kubwa ya wewe kupata angalau dakika tano kwa siku, kila siku kutafakari maisha yako na ya dunia kwa ujumla.

Kwa dunia ya sasa, mtu akipata hata dakika tano, atakimbilia kushika simu na kuangalia ni vitu gani vinampita kwenye mitandao ya kijamii. Hali hii imekuwa inaongeza msongo wa mawazo na watu kushindwa kutafakari kile wanachofanya na kule wanakokwenda.

Ndio maana nimekuambia kama unaona huna muda wa kusoma hapa, basi wewe unahitaji kusoma mara mbili kwa sababu hali yako ni ngumu zaidi. Ni ngumu sana kama unakosa dakika 5 za kuacha kila kitu kwenye dunia kiende na wewe kukaa na kufikiri kwa kina juu ya maisha haya.

Hakikisha kila siku unapata muda wa kuwa na wewe mwenyewe, muda wa kujifunza na kutafakari kuhusu maisha na kuhusu kile unachofanya. Na pia pata muda wa kukaa kimya tu, usikimbilie simu au kuongea na wengine, kaa pale kwa dakika chache na pumua. Kupata muda wa kupumua na hapa namaanisha kupumua sawasawa ni tiba nzuri kwa changamoto nyingi.

Endelea kusoma makala hizi kila siku, na usisome kwa kukimbia, soma taratibu mpaka upate ujumbe, mpaka utoke na kitu cha kufanyia kazi, kwa sababu kila makala ina kitu hiko.

Kama bado hujapata kitabu KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO unasubiri nini? Unakosa nafasi nzuri ya kuwa na maisha bora. Tuma tsh elfu kumi kwenye namba 0717396253 au 0755953887 na kisha tuma email yako na utatumiwa kitabu. Hakikisha unapata muda kila siku wa kutafakari maisha.

SOMA; Ndio, hakuna jipya, lakini bado unahitaji kujifunza “KILA SIKU”.

TAMKO LANGU;

Nimejua ya kwamba maisha haya ya mwendokasi tunayokwenda nayo, siyo mazuri kwangu. Kwa sababu kuwa kwenye mbio tu ambazo sipati muda wa kutafakari, naweza kuwa napotea huku nazidisha mbio. Kuanzia sasa nitahakikisha napata muda wa kutafakari kila siku, hata kama ni kwa dakika tano tu, najua hizi ni bora kuliko kukosa kabisa.

NENO LA LEO.

Life goes by fast. Enjoy it. Calm down. It’s all funny. Next. Everyone gets so upset about the wrong things. – Joan Rivers

Maisha yanakwenda kasi. Yafurahie. Tulia. Kila mtu anavurugwa na vitu visivyo vizuri.

Pata muda wa kutulia na kutafakari maisha yako na kile unachofanya, usikubali kumezwa na mwendo kasi wa maisha ya sasa, utapotea.

Rafiki na Kocha Wako,

Makirita Amani,

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

TUPO PAMOJA.