Kuna wakati tunasahau ni kipi muhimu sana kwenye kufikia malengo yetu na mafanikio pia.

Tunaweka juhudi zetu kwenye mambo ambayo yanaweza kuonekana ni muhimu lakini kwa uhalisia sio muhimu.

Kwa mfamo, tunapoweka malengo na mipango, kuna maandalizi na kufanyia kazi malengo na mipango hiyo. Lakini watu wengi wamekuwa wakiweka muda mwingi kwenye maandalizi kuliko kwenye kufanya.

Maandalizi ni muhimu sana, lakini siyo sehemu muhimu ya ufanyaji. Unahitaji kujiandaa, lakini usihesabu ni sehemu kubwa ya kufanya. Wengi wa wanaotumia muda mwingi kujiandaa huona wamekamilisha sehemu kubwa sana. Lakini sio kweli, huwezi kuipima sehemu hiyo.

Pamoja na kuweka muda kwenye upangaji, unahitaji kuweka muda mwingi zaidi kwenye ufanyaji, maana hiko ndio kitu pekee utakachoweza kukipima, na kitakachokufikisha kwenye mafanikio makubwa.

Weka muda zaidi kwenye kufanya, na usiichie tu kupanga.

SOMA; Usipoteze Muda Kwenye Maandalizi, Anza Hivi..

TAMKO LANGU;

Nimejua ya kwamba kupanga na kufanya ni vitu viwili tofauti. Kupanga ni muhimu lakini hakuchukui nafasi ya kufanya. Pamoja na kupanga, ni muhimu kuweka muda zaidi kwenye kufanya kuliko kupanga. Kwa sababu kupanga hakuhesabiki, wala hakunifikishi kwenye mafanikio ninayotaka.

NENO LA LEO.

There are no secrets to success. It is the result of preparation, hard work, and learning from failure.

Colin Powell

Hakuna siri kubwa ya mafanikio. Mafanikio ni matokeo ya maandalizi, kufanya kazi kwa juhudi na kujifunza kutokana na makosa yako.

Maandalizi ni sehemu muhimu, lakini kufanya ni muhimu zaidi. Weka muda mwingi kwenye kufanya, usiishie tu kupanga.

Rafiki na Kocha Wako,

Makirita Amani,

makirita@kisimachamaarifa.co.tz

TUPO PAMOJA.