Kuna aina mbili za kushindwa kwenye biashara na katika aina hizo mbili kuna moja ambayo ni bora kwako na nyingine siyo bora.
Aina ya kwanza ya kushindwa kwenye biashara ni kuanzisha biashara halafu biashara hiyo ikafa. Hapa unajipanga na unaingia kwenye biashara ukiwa na malengo na mipango mizuri ila biashara yako haidumu muda mrefu, inakufa.
Aina ya piki ya kushindwa kwenye biashara ni kutokuingia kwenye biashara kabisa. Hapa kila unapoweka malengo na mipango ya kuingia kwenye biashara unashindwa kuingia kutokana na sababu mbalimbali ambazo kwako unaona zinafaa. Huku nako ni kushindwa kwenye biashara.
Ni aina ipi bora kwako?
Naamini jibu unalo.
Ni bora kuingia kwenye biashara na ukashindwa kuliko kutokuingia kwenye biashara kabisa.
Ni kweli ukishindwa unaumia kutokana na fedha na muda utakaokuwa umewekeza kwenye biashara hiyo. Lakini maumivu haya hayapiti hivi hivi, unajifunza kitu kikubwa sana ambacho kitakusaidia baadaye kwenye biashara.
Kutokuingia kwenye biashara kabisa unaweza kuona umejikomboa lakini umeshindwa vibaya sanam maana hakuna unachojifunza zaidi ya kuendelea kujijaza hofu zako.
Kwa vyovyote vile ingia kwenye biashara, kama hujaanza biashara yoyote anza sasa, huna cha kupoteza na una mengi ya kujifunza.
Karibu tujadiliane hapo chini kama una swali au changamoto yoyote inayohusiana na biashara.
#Kocha.