Inapokuja kwenye swala la upangaji wa bei za bidhaa au huduma tunazotoa, wafanyabiashara wengi wamekuwa wakifanya kwa mazoea.
Kuna hali fulani imezoeleka kwamba mteja ataomba kupunguziwa bei na ili kuhakikisha anapata faida, mfanyabiashara anaanza kumtajia mteja bei kubwa ili wakipunguzana bei irudi kule kwa kawaida.
Haya ni mazoea ambayo siyo mazuri kwa sababu wateja wanajijengea hadithi isiyo nzuri juu ya biashara yako. Mteja kila akija kwako atakuwa ameshajijengea hali kwamba ni lazima bei utakuwa umeweka juu. Na hata baada ya kuomba kupunguziwa, bei ile utakayokubaliana naye, bado moyoni atajilaumu kwamba angeshusha zaidi. Hii itamjengea mteja kutokukuamini na bei yoyote atakayolipa ataona umemlangua, labda kama angeanzia chini zaidi angepata.
Ufanye nini?
Mwambie mteja bei halisi ya bidhaa au huduma anayotaka na mshawishi kununua kwa bei hiyo. Usiongeze bei ili mkipuguza iwe sawa, na pia usilazimike iupunguza sana kama haitakulipa. Ijenge biashara yako katika misingi ya uaminifu na wateja watajisikia salama kufanya biashara na wewe.
Kila la kheri.
Kama una changamoto yoyote ya kibiashara ambayo ungependa tuijadili weka maoni yako hapo chini.