Mafanikio kwenye biashara siyo kitu rahisi, ila yanawezekana kama kweli ukijitoa.
Na ninaposema kujitoa namaanisha kujitoa kweli kwenye kuifanya biashara yako.
Leo nataka kukuambia, pumua biashara yako.
Kwa nini upumue biashara yako?
Kwa sababu pumzi ndio kitu ambacho huwezi kutengana nacho hata kwa dakika ukabaki salama.
Hivi ndivyo ilivyo kwa biashara yako, unahitaji kuifikiria biashara yako muda wote.
Kila unapokuwa fikiria ni fursa zipi unazoweza kuzitumia kwa biashara yako.
Unapokutana na watu wapya fikiria ni jinsi gani biashara yako inaweza kuwasaidia watu wengine.
Ijue biashara yako nje ndani, jua kila kitu kinachohusiana na biashara hiyo. Jua mwenendo wa biashara yako na kuwa mfuatiliaji mkubwa wa yanayoendelea kwenye biashara hiyo.
Na ili uweze kuipumua biashara yako lazima iwe ni kitu ambacho unakipenda sana. Kitu ambacho upo tayari kukizungumzia muda wote.
Ndiyo maana unahitaji kupenda sana biashara yako.
Je unaipumua biashara yako?