Watu wengi wanaofikiri wanatangaza biashara zao, ukweli ni kwamba wanapiga kelele.
Kabla hatujaendelea ni vyema tukajua kelele ni nini, ili tuone unahusianaje na wale wanaotangaza biashara.
Kelele ni sauti zisizo na mpangilio au sauti zisizohitajika kwa mahali husika au wakati husika.
Wafanyabiashara wengi wamekuwa wakiwapigia watu wengi kelele kuhusu biashara zao.
Wakekuwa wakikazana kumtangazia kila mtu kuhusu biashara zao. Hizi ni kelele kwa sababu wateja wako sio kila mtu.
Njia bora ya kutangaza biashara yako ni kuwajua kwanza ni watu gani wanaoweza kuwa wateja wako.
Jua watu hawa wanapatikana wapi na unawezaje kuwafikia.
Ukishajua hili sasa ndiyo unaweza kutengeneza njia bora ya kuitangaza biashara yako.
Ambapo taarifa zako zitawafikia wahusika, wale ambao wanajali kuhusu biashara yako na utaweza kuongeza wateja wako.
Usiendelee tena kupiga kelele, tumia vyema rasilimali zako kuhakikisha unawafikia walengwa.
TUPO PAMOJA.