Kuanzisha biashara ni rahisi, rahisi mno, unaweza kuanza biashara hata leo hii.

Lakini kuanza biashara ambayo itakuwa endelevu na yenye mafanikio makubwa ni kazi ngumu sana.
Ni ngumu kwa sababu kuna changamoto nyingi sana kwenye uendeshaji wa biashara yoyote ile.
Na ugumu unaendelea kuwepo hata kama utakuwa na mtaji mkubwa na kuweka muda wako wote mwenye biashara yako.
Kuna mambo mengi yanakuhitaji wewe kufanya maamuzi ambayo hujawahi kufundishwa popote.
Ndiyo maana ni muhimu sana kwako kama mfanyabiashara kuijua biashara yako vizuri.
Ijue biashara yako nje ndani, na endelea kujifunza kila siku kuusu biashara.
Na kila changamoto unayokutana nayo kwenye biashara itumie kama darasa. Usiiache ipite tu au usiishie kulalamika pekee, bali chukua hatua na ondoka na somo ambalo utalitumia kwenye  maamuzi yako ya kibiashara baadaye.
Kadiri unavyokutana na changamoto nyingi, kadiri unavyofanya makosa mengi, ndivyo unavyojifunza na kuwa bora.
Biashara ni kufanya, siyo kupanga wala kuanza, wengi wanaweza kupanga biashara, wengi wanaweza kuanza biashara, lakini ni wachache wanaoweza kufanya biashara na kufikia mafanikio makubwa.
Najua wewe ni mmoja kati ua hao wachache, endelea kuweka juhudi.
Kila la kheri.