Kitu ambacho watu wengi wanasahau kwenye safari hii ya mafanikio ni kwamba itakuchukua muda. Itakuchukua muda kuweza kutoka hapo ulipo sasa na kufika kule unakotaka kufika. Siyo kitu cha usiku mmoja, kwamba umelala masikini na kuamka tajiri.

Hii ni kwa sababu umetumia muda mwingi kujitengeneza vile ulivyo sasa. Mpaka sasa umetumia miaka mingi kujitengeneza ulivyo sasa. Hivyo kubadilika na kufanya makubwa, unahitaji muda wa kuondoa hayo uliyozoea mpaka sasa, na kutengeneza mapya yatakayokufikisha unakotaka.

Kama umefanya kazi miaka kumi na kikubwa unachoweza kuonesha ni madeni, hakuna namna unaweza kufuta hilo mapema, unahitaji muda wa kujitoa kwenye madeni yako na kujijengea nidhamu ya fedha, pamoja na kuongeza kipato chako.

SOMA; UCHAMBUZI WA KITABU; Getting Results The Agile Way (Mbinu Za Kuwa Na Matumizi Mazuri Ya Muda Na Kupata Ufanisi Mkubwa.)

Kama umefanya biashara miaka kumi lakini hutengenezi faida kubwa ya kuweza kuikuza biashara hiyo, badala yake unapata tu fedha ya kusukuma maisha, unahitaji muda wa kubomoa hicho ulichojenga na kuanza kujenga biashara ya tofauti itakayokuletea mafanikio.

Ni lazima ujipe muda kwa sababu hujafika hapo ulipo kwa ajali, ulitumia muda kujijenga ulivyo, unahitaji muda kubomoa hicho ulichojenga mpaka sasa, na kujenga kile unachotaka.

Mipango yote unayopanga kwenye maisha yako, ipe muda na kuwa mvumilivu, hakuna jambo zuri linalotokea kwa haraka kama ajali, unahitaji kujenga kama ulivyojenga sasa.

Kila la kheri.

TUPO PAMOJA,

KOCHA MAKIRITA AMANI.

www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita

Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)