Hakuna ubishi kwamba kila mmoja wetu anaweza kuwa bora zaidi ya alivyo sasa, anaweza kuongeza kipato chake zaidi ya alichonacho sasa, bila ya kutegemea kwa sasa yupo chini au juu kiasi gani. Kila mmoja wetu ana nafasi ya kuwa bora zaidi, kufanikiwa zaidi.
Lakini hili nalo linakuja na changamoto yake. Wengi wamekuwa wakitumia muda mwingi kufikiria kule wanakotaka kufika na kusahau pale walipo sasa. Wengi wamekuwa wakiangalia kule wanakotaka kwenda na kufikiria ni namna gani wanaweza kufika kule. Wanasahau kabisa pale walipo sasa na hivyo kukosa fursa kubwa y akufika wanakotaka kufika.
Unaweza kufika kokote unakotaka kufika, lakini lazima utaanzia hapo ulipo sasa. Hapo ulipo ndipo penye nafasi nzuri kwa wewe kuanzia. Kazi unayofanya sasa ndiyo sehemu nzuri ya kuanzia maisha yako ya mafanikio, hata kama kazi hiyo siyo nzuri na bora kwako. Biashara unayofanya sasa ndiyo sehemu nzuri kwako kuanzia safari yako ya mafanikio, hata kama biashara hiyo haiendi vizuri kama ulivyokuwa umepanga.
SOMA; Ni Afadhali Kupotea Kuliko Kubaki Hapo Ulipo.
Hapo ulipo kuna mengi ya kukuwezesha kusonga mbele, hapo ulipo kuna fursa nyingi unazoweza kuzitumia kubadili na kuboresha maisha yako. fikiria vyovyote utakavyo, weka malengo makubwa utakavyo, lakini usisahau kuyahusisha na hapo ulipo sasa. Kama utadharau hapo ulipo sasa, utaishia kuwa mtu wa mipango pekee, hutaweza kupiga hatua yoyote kubwa.
Anzia hapo ulipo sasa, kuna nafasi kubwa ya wewe kupata njia ya kuelekea kule unakotaka.
TUPO PAMOJA,
KOCHA MAKIRITA AMANI.
www.kisimachamaarifa.co.tz/makirita
Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)