Habari za leo rafiki yangu,
Karibu tena kwenye mazungumzo yetu ya leo ambapo mimi na wewe rafiki yangu tunashirikishana yale muhimu kwa maisha yetu ya mafanikio.
Leo nina mengi ya kukushirikisha lakini tutaanza na moja muhimu sana ninalotaka ulijue na kulisimamia kila siku kwenye maisha yako. Kwa kujua hiki na kukisimamia, hakuna ambacho kitakushinda kwenye maisha yako. Hiki ninachokwenda kukushirikisha leo ndiyo kimebeba ujumbe mzima ambao nimekuwa nakushirikisha kila siku kupitia kazi mbalimbali ninazofanya.
Kitu kimoja, ambacho nataka wewe rafiki yangu ukijua na kukiishi kila siku ni hiki; MFAFANIKIO NI HAKI YAKO YA KUZALIWA. Kama ilivyo kwamba kuishi ni haki yako ya kuzaliwa, hivyo ndivyo mafanikio pia yalivyo. Una haki ya kufanikiwa na hakuna mwingine ambaye anaweza kukuondolea haki hiyo. Kama unaishi basi una haki ya kufanikiwa.
Kama ilivyo kwa haki nyingine, haki yako ya kufanikiwa haitakamilika kama wewe hutaifanyia kazi. Ni sawa na haki ya kuishi, ndiyo una haki ya kuishi lakini kama hutalinda afya yako hutaweza kuishi. Kama utakula hovyo na hutojali kuhusu magonjwa, utakufa haraka japokuwa una haki ya kuishi.
Hivi pia ndivyo ilivyo kwenye haki yako ya kufanikiwa. Kama wewe mwenyewe hutachukua hatua madhubuti za kufanikiwa, haki hii hutaweza kuifurahia. Kama utaishia kuwalalamikia na kuwalaumu wengine, kama utaishia kuona wengine ndiyo wanaokukwamisha, hutapiga hatua yoyote kubwa.
Ndiyo maana leo hii nakuambia wewe rafiki yangu, haki yako hii ya kuwa na maisha ya mafanikio, maisha bora na yenye furaha, ni jukumu lako mwenyewe. Ni lazima uchukue hatua za makusudi ili uweze kufurahia haki hii uliyonayo.
Kuna usemi kwamba haki haiombwi bali inachukuliwa au inadaiwa. Ni usemi ambao una nguvu na una ukweli ndani yake. Ukiomba haki ni vigumu sana kupewa, lakini unapoichukua haki au kudai haki, unapewa. Hivi pia ndivyo ilivyo kwenye mafanikio, mafanikio hayaombwi, mafanikio yanatafutwa, mafanikio yanafanyiwa kazi.
Hakuna njia yoyote rahisi na ya mkato ya kufikia mafanikio, ni lazima tayari kuweka juhudi kubwa ili uweze kufanikiwa, bila ya juhudi, hata ungeongea kiasi gani kwamba unataka kufanikiwa, hutayaonja mafanikio. Sijui unanielewa rafiki yangu? Nataka leo uondoke na hili muhimu na ulifanyie kazi kila siku, kwa sababu hakuna mwingine atakayekazana na mafanikio yako zaidi ya wewe mwenyewe unavyokazana nayo.
Swali muhimu ni je, ni juhudi gani ambazo unaendelea kuweka kila siku ili kuhakikisha unakuwa na maisha ya mafanikio? Siyo maneno, bali juhudi gani?
Kama nilivyotangulia kusema, nina mengi ya kukushirikisha;
Jana nilipata nafasi ya kukutana na Coach James Mwang’amba. Ulikuwa ni mkutano mzuri sana na kuna mengi mno ambayo tulishirikishana.
Nina hakika utakuwa unamjua Coach James, kwa sababu amekuwa kwenye kazi hii ya ukocha kwa muda mrefu, kabla ya wengi wetu. Amekuwa mzungumzaji na mhamasishaji na amekuwa anaendesha mikutano na makongamano ya mafunzo ya biashara, uchumi na ujasiriamali.
Tulizungumza mengi kuhusu fursa za kibiashara, ambazo tutaendelea kushirikishana kwenye kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA, hapa nitakushirikisha kitu kimoja muhimu mno. Kila mtu kuna namna unaweza kuongeza thamani kwake, na mara nyingi mtu huyo hatakuambia ni thamani gani anahitaji, lakini udadisi wako utakufanya uone thamani unayoweza kuongeza kwake.
Ni katika mazungumzo yetu na Coach James ambapo tulijadili mengi na hatimaye nikaona namna ya kuongeza thamani kwenye huduma anazozitoa, kitu ambacho kitatuwezesha kufanya kazi kwa pamoja.
Hivyo rafiki yangu, kitu kimoja ninachotaka kukukumbusha ni hiki, kwa mtu yeyote unayekutana naye, fikiria jambo hili moja, ni namna gani ninaweza kuongeza thamani kwake. Kwa kujiuliza hivi na kuwa mdadisi utaziona njia nyingi za kuongeza thamani kwa wengine kupitia kile ambacho wewe unafanya.
Baada ya mkutano ule Coach James alikuwa na haya ya kusema, picha iko hapo chini.

Kama hujaweza kuisoma picha basi maelezo yake ni haya;
Meeting two giants today was awesome. On my right, is my friend Amenye Mwakisambwe a top earner in one local based networking here in Tanzania, who is joining me in Onelife! He had 23,000 members in his downline. What a blessing.
Coach Makirita…on my right! Oh boy, this boy is up to something! Think about it; when he was in high school he got Division 1 with 3 points in his Form 6 results (Straight As i.e A in Biology, A in Physics and A in Chemistry). Though still a University student at Muhimbili he has mastered so many aspects of success through self study and personal development. For example
1. He wakes up everyday at 4PM to write for several years now. He has now written 6 books in PDF formats
2. Manages several blogs and long email list in his database
3. Manages his own reading club. If you are in his club, you have to read two books per week or you are out! No discussion
4. He leads an investment company with close to 50 investors.
5. He coaches people to solve different problems and helps entrepreneurs to develop blogs and websites
6. He has a goal to be a billionaire in his life time and national president by year 2040.
The last time I met a Tanzanian like him was about 3 years ago when I met Dr. Saed Saed who is now my friend and lives in Zanzibar. If you know someone like him (he is only 28) let me know him/her as soon as possible. When I heard about Coach Makirita last Friday night at 10.30 pm at night, I couldn’t wait, I called him immediately to ask to meet him.
I am always looking for people like him all over Tanzania. People with BIG dreams but with TREMENDOUS disciplines in action taking!
Follow him up on these blogs to learn about his programs; www.amkamtanzania.com and www.kisimachamaarifa.co.tz
Contacts; +255 717 396 253 / makirita@kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT (His success motto).
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Kwa ushauri na Coaching bonyeza maandishi haya kupata utaratibu.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea MOBILE UNIVERSITY (bonyeza hayo maandishi.)
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea MTAALAMU NETWORK