Habari za asubuhi ya leo rafiki yangu?
Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo, ambapo tumepata nafasi nzuri ya kwenda kuweka juhudi zaidi kwenye kile tunachofanya.
Hii ni nafasi ya kipekee rafiki yangu, tuitumie vizuri.

Asubuhi ya leo tutafakati kuhusu KUJIDHIBITI WEWE MWENYEWE.
Watu wengi wamekuwa wakikazana kutafuta mbinu za kuwadhibiti watu wengine, lakini wamekuwa wakishindwa kufanya hivyo. Wanahangaika saha lakini hawafanikiwi kwa sababu hawajui mtu sahihi kwao kumdhibiti ni yupi.
Mtu sahihi kwako kumdhibiti ni wewe mwenyewe.
Ukitaka kuwadhibiti wengine, anza kujidhibiti wewe mwenyewe.
Yule awezaye kujidhibiti, anaweza kuidhibiti dunia nzima.
Hii ni kwa sababu dunia inakujibu kwa kile unachofanya. Unapojidhibiti, dunia nayo inajidhibiti ili iweze kwenda na wewe.

Anza kujidhibiti mwenyewe, anza kujijengea nidhamu kwenyewe, anza kujiwekea miiko mwenyewe na dunia itakufuata kwa uekekeo wako.

Nakutakia siku njema sana rafiki yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
http://www.makirita.info

img_20161027_071957