Leo ni siku bora na ya kipekee sana kwetu,
Ni siku ambayo tumekuwa tunaisubiri ili kuweza kufanya makubwa kwenye maisha yetu. Tusiahirishe tena yale tuliyopanga leo, kwa sababu hayuwezi kupata siku bora kama hii tuliyopata leo.

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu MIMI MWENYEWE…
Nipo hapa nilipo sasa kwa sababu MIMI MWENYEWE nimependa kuwa hapa.
Kipato ninachopata sasa ni kwa sababu MIMI MWENYEWE nimeamua nipate kipato hichi.
Marafiki nilionao kwenue maisha yangu ni MIMI MWENYEWE nimechagua kuwa nao.
Matatizo yote ninayopata kwenye maisha yangu ni MIMI MWENYEWE nimeyachagua na kuyakubali kwenye maisha yangu.
Mafanikio makubwa ninayotaka kwenye maisha yangu ni MIMI MWENYEWE ambaye nahitaji kuyaruhusu yatokee kwenye maisha yangu.
Kazi/biashara ninayofanya sasa, ambayo hainipi kile ninachotaka, ni MIMI MWENYEWE nimeichagua na kuendelea kuing’ang’ania.
Najua kabisa mwamuzi wa mwisho wa maisha yangu, na mtu pekee wa kulalamikiwa na kulaumiwa kwa chochote kinachoendelea kwenye maisha yangu ni MIMI MWENYEWE.
Hivyo basi, leo hii naianza siku yangu, nikikiri ya kwamba, leo na kila siku ya maisha yangu ni zao la MIMI MWENYEWE nitakavyoipeleka siku yangu.
Hii ndiyo hatua ya kwanza na muhimu kabisa ya mimi kufikia mafanikio makubwa na kupata chochote ninachotaka. Ninapoamua kushika hatamu ya maisha yangu, hakuna chochote kinachoweza kunizuia.
Nakutakia siku njema sana rafiki yangu, KAFANYE MAKUBWA SANA LEO.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
http://www.makirita.info
ujumbe mzuri tena kwa kiswahili fasaha,,,, ahsante
LikeLike
Asante sana.
LikeLike