Hongera rafiki kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Leo tumepata nafasi nyingine ya kipekee ya kwenda kuweka juhudi kubwa ili tuweze kupata matokeo bora sana.
Tutumie siku hii ya leo vizuri rafiki yangu, ili tuweze kufikia malengo yetu.

img_20161112_091656

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu mengi ya kufanya.
Kwa wakati wowote ule, kila mmoja wetu anayo mambo mengi sana ya kufanya.
Yapo mambo mengi yanayotaka muda wako.
Kila dakika ya maisha yako, inagombaniwa na vitu vingi ambavyo unahitajika kufanya.
Lakini siyo vitu vyote ni muhimu kwako kufanya.

Kadiri unapokuwa na mambo mengi ya kufanya, ndivyo unavyojikuta unashindwa kufanya hata jambo moja kwa usahihi. Kama utayafikiria yote unayotaka kufanya, unaweza kukata tamaa na ukashindwa kabisa kuanza kufanya.
Unaweza kujikuta unatumia muda mwingi kuamua ni lipi uanze kufanya, na mpaka uje kufikia kufanya, umeshachoka kiakili.

Ufanye nini?
💥Kila siku chukua kalamu na karatasi na orodhesha mambo yote unayotaka kufanya.
💥Yapange jambo hayo kwa umuhimu wake, lile muhimu zaidi lipe namba moja, endelea mengine mpaka la mwisho.
💥Anza kufanya lile ambalo ni namba moja, na usifanye lingine mpaka unemaliza hilo namba moja.
Kuwa na nidhamu kubwa sana kwenye hili.

Nakutakia siku njema sana ya leo rafiki yangu.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
http://www.makirita.info