Hongera rafiki kwa siku nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo makubwa.
Tumia muda wako wa leo vizuri rafiki, ili uweze kufanya makubwa kwenye maisha yako.

img_20161112_091656

Asubuhi hii tutafakari kuhusu urahisi wa mafanikio.
Moja ya vitu ambavyo wengi wamekuwa wanalalamika ni ugumu wa mafanikio.
Utakuta mtu analalamika biashara ni ngumu mno. Au inakiwa vigumu kwake kufanikiwa kwa kile anachofanya.

Rafiki, kitu kinapokuwa kigumu ndipo unapaswa kufurahi zaidi kwa sababu ugumu ndiyo unaongeza thamani.
Ingekuwa rahisi kila mtu angefanya na hivyo ushindani ungekuwa mkubwa.
Ugumu unawaondoa wavivu na wale ambao hawajajitoa kweli, unawaacha wale ambao wamechagua hata kama ni magumu kiasi gani.

Tunaweza kusema ni rahisi kufanikiwa kwenye jambo gumu kuliko kwenye jambo rahisi. Kwa sababu jambo rahisi kila mtu analifanya.
Hivyo rafiki, usilalamikie mambo magumu, badala yake yapokee na yatumie kufanikiwa.

Nakutakia siku njema sana rafiki yangu.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
http://www.makirita.info