Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kufanya makubwa ili siku yetu ipate kuwa bora sana.
Tumianjuda huu ulioupata leo vizuri rafiki yangu, maana hutokuja kuupata tena.

img_20161112_091656

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu ZAIDI KIDOGO…
Watu wengi wanapofikiria kufanya kitu, huwa wanaangalia hatua za juu kabisa. Wanawaangalia wale ambao wameshapiga hatua kubwa na kutaka kuwa kama wao, haraka sana.
Wanapoianza safari, ndipo wanagundua ya kwamba mambp siyo rahisi kama walivyokuwa wanafikiria. Vikwazo ni vingi na kwenda mbele ni kugumu. Hapa ndipo wengi wanapokata tamaa na kuona haiwezekani.

Sasa leo unahitaji kubadili mtazamo wako kuhusu kile unachofanya, kuhusu kule unakotaka kufika. Usianze na tamaa ya makubwa, badala yake unahitaji kupiga hatua kidogo, kila siku.
Unahitaji kufanya jambo bora kidogo zaidi ya ulilofanya jana.
Na kadiri unavyokwenda hivi, ndivyo unavyojiweka kwenye nafasi ya kupata makubwa.

Kila mmoja wetu anaweza kufanya zaidi kidogo kila siku.
Kuongeza juhudi zaidi kidogo,
Kuwa na uvumilivu zaidi kidogo,
Na kama unaweza kufanya zaidi kidogo, basi unaweza kurudia hili kila siku na hatimaye kufika kule unakotaka kufika.

Leo FANYA ZAIDI KIDOGO….

Nakutakia siku njema sana ya leo rafiki yangu.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
http://www.makirita.info